KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 1, 2012

SIMBA NA YANGA SASA KUCHEZA BancABCS Super8.



Hatimaye Vilabu vya Simba na Yanga vimekubali kushiriki michuano ya BancABC super8 iliyotambulishwa hivi karibuni mbele ya waandishi wa habari.
Michuano hiyo mpya ambayo hapo kabla iliingia katika utata mkubwa juu ya kukubaliwa kwake na vilabu hivyo vikubwa hapa nchini kutokana na kutokueleweka vizuri juu ya maslahi yao ikiwemo suala zima la zawadi mbali na wao kama vilabu watapata nini katika ushiri wao.

Wakiongea kwa nyakati tofauti na Rockersports mara baada ya kikao kilichoitishwa na TFF kuzungumzia juu ya hilo hii leo, viongozi wa vilabu hivyo viwili makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu na katibu wa Yanga John Celestine Mwesigwa wamesema kilichokuwa kinawapa tabu ni nini kilichomo ndani ya mkataba huo ambao uliingiwa baina ya TFF na BancABC kwa faida ya vilabu hivyo shiriki.

Makamu mwenyekiti wa Simba Kaburu amesema suala kubwa sio kukubali au kukataa kucheza katika ligi hiyo ndogo ya Super8 bali wao kama wadau hawakupata nafasi ya kuhusishwa wakati wa kuingia huo mkataba lakini sasa wamefikia makubaliano baada ya kuambiwa juu ya masuala ya msingi waliyokuwa wanayahitaji lakini wao pia wametoa angalizo juu ya maandalizi yao ya ligi kuu ya Vodacom kuvurugwa na ratiba ya mashindano hayo.

Amesema wao kama Simba kimsingi wamekubali kucheza katika ligi hiyo lakini watawatumia wachezaji wao wa kikosi cha pili cha under 20 wakiwachanganya na wachezaji wao wapya waliosajili msimu huu na wale ambao wanafikiria kuwasajili.

Kuhusu suala la zawadi Kaburu amesema kimsingi wamekubali zawadi itolewe kwa bingwa pekee lakini kuna mambo mengine muhimu wamekuwa bado wanajadiliana na TFF ambayo yatatolewa ufafanuzi na TFF baada ya kujadiliana na wadhamini wa ligi hiyo BancABC.
Kwa upande wao mabingwa wa kombe la kagame Yanga kupitia kwa katibu wao Mwesigwa Celestine wamesema wamekuwa wakiendelea na mjadala na TFF na mazungumzo yao na TFF yanaendelea vizuri.
Amesema kimsingi watafikia muafaka juu ya hilo kwa kuwa mjadala umefikia katika hatua nzuri na taarifa itatolewa juu ya nini kimefikiwa baina ya pande zote tatu yaani TFF,BancABC na vilabu vyote.
Hata hivyo hakuwa tayari kuzungumzia ni wachezaji gani watakao watumia katika ligi hiyo mpya
TFF imezitaja timu za Tanzania bara za Simba,Yanga na Azam kama timu zilizoshika nafasi za juu katika msimu uliopita wa ligi kuu ya Vodacom pamoja na timu moja iliyopanda daraja la kwanza kushiriki ligi hiyo ambapo watakuwa wakiungana na vilabu vya Zanzibar vyenye matokeo yanayo fanana na hayo.

Michuano hiyo ya BancABC SUP8R soccer Tournment 2012 imepangwa kwa mtindo wa makundi mawili na itachezwa kwenye miji ya Dare s salaam, Mwanza , Arusha na Zanzibar na imepangwa kuanza August 4.

No comments:

Post a Comment