WACHEZAJI
17 WAPINGWA KWENYE USAJILI
Klabu
mbalimbali zimewasilisha pingamizi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kupinga usajili wa wachezaji 17 walioombewa usajili katika timu za Ligi Kuu.
Toto
Africans ya Mwanza imewawekea pingamizi wachezaji Enyinna Darlinton aliyeombewa
usajili Kagera Sugar, na Mohamed Soud anayekwenda Coastal Union kwa maelezo
kuwa bado ina mikataba na wachezaji hao.
Pia
Flamingo ya Arusha inapinga usajili wa wachezaji wake Kelvin Friday Iddy katika
timu za Azam na Salim Walii (Polisi Mara) kwa vile taratibu za kuwahamisha bado
hazijafanywa. Nayo Kagera Sugar inapinga usajili wa beki David Charles Luhende
kwenda Yanga kwa vile ada ya uhamisho haijalipwa.
Super
Falcon ya Chanjamjawiri, Chakechake, Pemba inapinga wachezaji wake wanne;
Edward Christopher Shija, Samir Said Luhava (Simba), Robert Joseph Mkhotya
(African Lyon) na Sultan Juma Shija (Coastal Union) kusajiliwa katika timu hizo
kwa maelezo taratibu halali za uhamisho hazikufuatwa.
Mchezaji
Othman Hassan aliyeombewa usajili Coastal Union anapingwa na Oljoro JKT kwa
vile bado ana mkataba na timu hiyo unaomalizika Mei 24, 2013. Nayo Rollingstone
Multipurpose Ateclass Foundation ya Arusha inapinga usajili wa Kigi Makassy
kutoka Yanga kwenda Simba hadi itakapolipwa fidia ya kumlea mchezaji huyo kwa
vile bado hajafikisha umri wa miaka 23.
Azam
inapinga usajili wa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenda Simba kwa maelezo bado ina
mkataba naye unaomalizika Juni 11 mwakani. Nayo Simba inapinga Kelvin Yondani
kusajiliwa Yanga kwa maelezo kuwa ina mkataba naye uliosainiwa Desemba 23 mwaka
jana.
Vilevile
Simba imewasilisha malalamiko ya mchezo usio wa kiungwana katika usajili wa
Mbuyu Twite aliyeko Yanga kwa maelezo alisaini mkataba na klabu yao Agosti Mosi
mwaka huu mbele yao, viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA)
na APR ambapo alilipwa dola 30,000 na nyingine 2,000 ikiwa ni fedha ya kujikimu
na nauli yake ya kujiunga na klabu hiyo.
Nayo
Yanga inapinga Simba kuwaacha wachezaji Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu
Mbiyavanga na Lino Masombo kwa maelezo walishapatiwa leseni za kucheza Ligi ya
Tanzania walizozitumia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame. Pia inapinga
Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kujiunga Simba kwa vile ana leseni ya kuchezea Azam
kwa msimu wa 2012/2013.
Pingamizi
lingine la Yanga kwa Simba ni kuwa imezidisha idadi ya wachezaji wa kigeni
wanaotakiwa kusajiliwa kwa maelezo inao wanane wakati wanaoruhusiwa ni watano.
Imewataja wachezaji hao kuwa ni Lino Masombo, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mussa
Mude, Kanu Mbiyavanga, Pascal Ochieng, Komalmbil Keita na Daniel Akuffor.
Kamati
ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Alex
Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia pingamizi
hizo pamoja na usajili wa wachezaji kwa ujumla kwa 2012/2013.
No comments:
Post a Comment