Amri katikati akiwa naSelemani Mtola katika benchi la timu ya Simba B |
KOCHA
msaidizi wa zamani wa timu ya Simba,Amri Said amepata ulaji baada ya kuingia
mkataba wa kuinoa timu ya KJ 94 inayo shiriki ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Akiongea na Rockersports kwenye uwanja wa Lugalo ambapo timu hiyo imekuwa ikifanya mazoezi yake kujiandaa na michuano hiyo inayotarajiwa kuanza hivi karibuni amesema, kimsingi
amekubali ofa ya timu hiyo na hivi sasa viongozi wa timu hiyo wanafanya mawasiliano na waajiri wake ambao ni klabu ya Simba ili aweze kupata baraka za uongozi wa klabu hiyo ambayo imempa kazi ya kuwepo kwenye benchi la ufundi la kikosi cha pili.
Said amechukua nafasi ya kocha Lucas Muhindi ambapo ameanza kuwanoa wachezaji 28 waliosajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya michuano hiyo na wamecheza michezo kadhaa na kufanya vizuri na yupo mbioni kutaka kuongeza wachezaji wanne katika kikosi hicho baadaya kugundua kasoro kadhaa .

Chini ya Amri Said, timu hiyo imeweza kucheza michezo kadhaa ikiwemo dhidi ya Villa na kushinda mabao 2-1,piailitoka sare na Pan Africa kwakufungana mabao 2-2,iliweza kuitandika timu ya Kinondoni Muslim kwa bao 1-0,ilitoka sare na Ruvu Shooting kwa bao 1-1.
Kabla ya kujiunga na 94KJ alikuwa akifundisha timu ya Ndanda Mtwara
No comments:
Post a Comment