Hodgson amekubali kwa shingo upande kustaafu kwa John
Terry timu ya Taifa
Meneja wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson ameonyesha
kusikitishwa kwake na hatua ya mlinzi wa kimataifa wa John Terry kustaafu soka
la kimataifa lakini amesema hana budi kukubaliana na maamuzi yake.
Nahodha huyo wa Chelsea ameamua kuachana na soka la
kimataifa jumapili usiku kuelekea katika kesi ya FA kusikiliza shauri dhidi yake la matumizi ya
lugha ya kibaguzi dhidi ya mlinzi wa QPR Anton Ferdinand October mwaka jana
huku akisema hakuna nafasi ya kuilinda tena nafasi yake katika timu ya Taifa.
Meneja huyo amemtakia kila la kheri mlinzi huyo katika
utumishi wake pale Stamford Bridge na kutanabaisha kuwa taarifa hizo amezipokea kwa mshtuko sana.
amenukuliwa akisema
"ningependa kumshukuru John Terry kwa namna
alivyo wajibika katika taifa lake la England tangu nianze kazi ya umeneja, kwa
kweli nimesikitishwa kumkosa mchezaji mwenye uzoefu na uwezo wa kimataifa kama John"
"ningependa kumtakia kila la kheri akiwa na klabu
yake ya Chelsea."
Kwa upande wa taarifa ya FA pia imeendana na maneno ya Hodgson
wakati ambapo Terry akiwa na rikodi ya kuwa nahodha katika kikosi cha Three
Lions mara mbili ndani ya kipindi cha mizengwe dhidi yake.
Taarifa ya FA imesomeka,
"kufuatia kutangaza kwake kutoka katika timu ya
taifa ya England, FA ingependa
kumshukuru John Terry kwa jitihada zake katika timu ya Taifa katika kipindi cha
miaka kumi iliyopita.
"katika kipindi cha uchezaji wake michezo 78 aliyo
itumikia timu ya Taifa John mara zote alijitoa kikamilifu katika timu."
Messi akanusha kuwa na matatizo na Villa
Lionel Messi amekanusha kuwa na matatizo na David
Villa baada ya kutoleana maneno katika mchezo wa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
Granada mchezo wa ligi kuu ya Hispania La Liga uliopigwa jumamosi, malumbano
ambayo yalinaswa na vyombo vya habari.
Katika mchezo huo uliopigwa Camp Nou, kabla ya
mapumziko na matokeo yakiwa 0-0, Messi, alikwaruzana na Villa baada ya kuharibu
shambulizi zuri wakiwa ndani ya eneo la hatari la Granada ambapo alionekana Messi
akimlalamikia Villa kwa kushindwa kumpasia pasi ya mwisho mapema akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga.
Television ya nchini Hispania ilirudia tukio hilo mara
kadhaa kutoka kona mbalimbali za uwanja jambo ambalo lilionekana kama tukio
kubwa kutokea baina yao.
Hata hivyo Messi
amesisitiza kuwa hakuna haja ya kulikuza tukio hilo ambalo limesha pita na
kudharau jambo hilo.
"kitu kama hicho hutoke katika mchezo, ni kitu cha kawaida,
utataka kufunga goli la kwanza na baadaye kila kitu kinakuwa kawaida . yanatoke
katika mazoezi lakini watu hawaoni hilo hivyo ni kitu cha kawaida"
"sina tatizo na ‘el Guaje’ yaani Villa, ni
kinyume na mnavyo fikiria. Historia yangu na yeye iko poa ndani ya chumba cha
kubadilishia nguo tuko poa, usitafute matatizo sehemu ambayo hakuna hilo,
tulikasirikiana kwasababu tulitaka kufanya vizuri na mazingira yanaweza
kukufikisha hapo."
No comments:
Post a Comment