Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
vyama vya mpira wa miguu mikoa ya Kilimanjaro (KRFA) na Manyara (MARFA)
katika uchaguzi uliofanyika juzi (Septemba 22 mwaka huu).
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza vyama hivyo unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KRFA na ule wa MARFA walivyo na imani kubwa
kwao katika kusimamia mchezo huo katika mikoa hiyo.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa kamati za utendaji za MARFA na
KRFA zinazoongozwa na Elley Mbise na Goodluck Moshi, kwani viongozi hao
wapya wana changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha wanaendesha
shughuli za mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba zao na vyombo vya mpira
wa miguu vilivyo juu yao.
Pia
tunatoa pongezi kwa kamati za uchaguzi za IRFA na MARFA na Kamati ya
Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa
kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa kuongoza MARFA ni Elley Mbise (Mwenyekiti), Wilson
Ihucha (Makamu Mwenyekiti), Apollinary Kayungi (Katibu), Peter Abong’o
(Mhazini), Khalid Mwinyi (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Phortinatus
Kalewa (Mwakilishi wa Klabu TFF) na Peter Yaghambe (Mjumbe).
Kwa
upande wa KRFA waliochanguliwa ni Goodluck Moshi (Mwenyekiti), Mohamed
Musa (Katibu), Kenneth Mwenda (Mwakilishi wa Klabu TFF), Kusiaga Kiyata
(Mhazini) na Denis Msemo (Mjumbe). Nafasi zilizowazi baada ya kukosa
wagombea wenye sifa kwenye vyama hivyo zitajazwa baadaye.
WASHABIKI 65,458 WAZISHUHUDIA SIMBA, YANGA WIKIENDI
Mechi
za Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara za Simba na
Yanga zilizochezwa wikiendi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zimeshuhudiwa
na washabiki 65,458.
Yanga
ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya JKT Ruvu, Jumamosi
(Septemba 22 mwaka huu) mechi yao ilishuhudiwa na washabiki 15,770
wakati ile ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa jana (Septemba 23 mwaka
huu) ilikuwa na washabiki 9,688. Simba ilishinda mabao 2-1.
Wakati
mechi ya Yanga iliingiza sh. 88,251,000 ile ya Simba dhidi ya Ruvu
Shooting Stars mapato yalikuwa sh. 55,454,000. Mechi ya Yanga kila timu
ilipata sh. 19,846,194.92 huku ile ya Simba kila timu ilipata
sh.11,350,774.58.
MECHI YA AZAM, MTIBWA SUGAR ZAINGIA MIL 2.5/-
Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyochezwa juzi
(Septemba 22 mwaka huu) Uwanja wa Chamazi imeingiza sh. 2,509,000 ambapo
kila timu imepata mgawo wa sh. 301,661.
Washabiki 827 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Nayo
mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Tanzania Prisons iliyochezwa
jana (Septemba 23 mwaka huu) kwenye uwanja huo imeingiza sh. 245,000
huku kila timu ikipata sh. 32,286. Prisons ilishinda mechi hiyo kwa
mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment