Ligi kuu ya Tanzania Bara imeendelea tena hii leo ambapo jumla ya timu sita zilikuwa uwanjani.
Katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Ruvu Shooting walikuwa ni wenyeji wa mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba, ambapo Simba wameendeleza rikodi yao nzuri ya ushindi msimu huu baada ya hii leo kuifunga Ruvu Shooting kwa mabao 2-1 huku mabao ya Simba yakiwekwa nyavuni na Felix Sunzu kunako dakika ya 29 ya mchezo bao ambalo lilitokana na krosi nzuri ya Nassoro Cholo ambayo ilizamishwa nayavuni kwa kichwa na Sunzu.
Bao hilo lilisawazishwa na mshambuliaji Seif Said kunako dakika ya 71 ya mchezo kufuatia makosa ya mlinzi wa Simba Juma Nyoso kuzembea kuunasa mpira ambao ulikimbiliwa na Seif Said na kuukwamisha wavuni.
Bao la pili la Simba na la ushindi lilifungwa na Edward Christopher baada ya kupokea pasi nzuri ya Mrisho Ngasa kunako dakika ya 85 ya mchezo huo.
MICHEZO YA MENGINE YA LEO
23.09.2012. MGAMBO JKT 0 VS 1 KAGERA SUGAR -MKWAKWANI TANGA
23.09.2012.
SIMBA 2 VS 1 RUVU SHOOTINGS- NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM 23.09.2012. 21
AFRICAN LYON 0 VS 2TANZANIA PRISONS -AZAM
COMPLEX DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment