Steven Akiwa mazoezi |
Steven George Lutego akiwa katika mazoezi na kocha wake wa ngumi Frank |
Huyu ndiye baba yake Steve, George Lutego 'Baunsa' |
Steven George Lutego ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 16 mwanafunzi wa kidato cha kwanza, mkazi wa Kurasini jijini Dar es Salaam mwenye dhamira ya kuiletea sifa Tanzania kwa kuleta medali ya dhahabu katika michezo ya Olympic ya Rio de janeiro nchini brazil Brazil mwaka 2016.
Dhamira ya Steven imejengwa na inaendelea kujengwa na baba yake George Lutego ambaye hapo zamani alikuwa ni mchezaji wa ngumi lakini hakuwa na sifa kubwa ya kuliletea Taifa hili lenye wingi wa vipaji ambavyo havichimbwi wala kutafutwa kama inavyotafutwa dhahabu na mafuta aridhini.
Akiongea na Rockersports Steven amesema amekuwa kila siku akipewa risala na baba yake George kuwa anataka kumuona akifanya mazoezi ya ngumi kila siku jioni isipokuwa jumapili tu kwa kuwa baba yake huyo anataka kuiona medali ya dhahabu mwaka 2016 iliwa imeletwa na mtoto wake.
Amesema baba yake amemnunulia vifaa vyote vya mchezo wa ngumi ikiwa ni pamoja na kumtengenezea ka-gym kadogo kwa ajili ya mazoezi yake lakini pia amekuwa amkienda katika viwanja vya wazi kufanya mazoezi yake.
Steven anasema baada ya kukubaliana na baba yake tayari amekuwa katika mazoezi ambayo imejengeka akilini mwake kiasi hata akiwa shuleni amekuwa anafikiria ndoto hiyo ya kwenda Brazil kuleta Medali.
Anamshukuru baba yake mzazi kwa kuona kipaji chaken cha ngumi sasa amemtafutia kocha ambaye ni mdogo wake Frank Lutego ambaye ni ambaye kila siku anachoma mafuta kutoka Gongo la Mboto kumfuata Steven uwanja wa taifa kumpa mazoezi.
Steven ana umri wa miaka 16, na mpaka Olympic ya Brazil itakapokuwa imefika ni wazi atakuwa ana umri wa miaka 20 umri ambao haswa ndio muafaka kwa kijana kutakata katika medali ya michezo.
Baba yake na Steven ambaye ni mwana michezo mzuri anafanya mazoezi ya ngumi kujiweka fiti katika mwili wake ameongea na Rockersports akisema yuko tayari kumpatia Steve kila kitu kinacho husu maandalizi yake kama alivyo anza ili kufanikisha ndoto yake yeye kama baba lakini sifa kwa kijana wake ambaye tayari ameanza kuonyesha mwelekeo mzuri katika mchezo huo.
Mdau mwingine ni wewe msomaji wangu, kama kuna kijana karibu yako awe mtoto wako, mtoto wa kaka, mtoto wa mjomba mtoto wa jirani vyovyote vile mwenye umri kama huo au unaofanana na huo yaani kuanzia miaka 13, 14, 15 na kuendelea na umegundua kuwa ana kipaji jaribu kumuweka wazi kwa kile alicho nacho na sema unakipaji cha aina fulani ili ajitambue ili awe na moyo.
Wasiliana na vyama vya michezo husika na eleza unacho kiona ili kuokoa kipaji chake huenda ata utajiri mkubwa ndani yake lakini hajitambui. Baba yake Steven, Geroge Lutego amekiona kipaji cha mwanae na anakiendeleza na wewe fanya sasa.
kwa maoni hapo chini.
No comments:
Post a Comment