MOURINHO: 'DNA' IMEREJEA REAL MADRID
Kocha wa Real
Madrid Jose Mourinho amepaza sauti yake iliyokuwa na nakshi za furaha baada ya
kikosi chake kilichokuwa mara kadhaa nyuma kimatokeo na baadaye kupata ushindi wa
mabao 3-2 dhidi ya mabingwa wa ligi kuu nchini England Manchester City katika
mchezo wa michuano ya vilabu bingwa barani ulaya uliopigwa katika dimba la Bernabeu.
Los Blancos iliyokuwa
nyuma kuelekea dakika za mwisho na ilipata mabao yake mawili ndani ya dakika tatu
za muda wa kawaida wa mchezo kupitia kwa Karim Benzema na Cristiano Ronaldo, na
kujihakikishia points tatu muhimu katika mchezo ambao ulikuwa mgumu usiku wa jana.
Amenukuliwa kocha
huyo na na kituo cha television cha ITV akisema
"ni
vizuri kwa kuwa 'vina saba' kwa wachezaji wangu vimerejea."
"Real
Madrid inaweza kupoteza mchezo , Mourinho anaweza kupoteza mchezo, wachezaji
wangu wanaweza kupoteza mchezo , na tungeweza kupoteza mchezo usiku huu.
Tungeweza kupoteza,
najivunia kwani tungeweza kupoteza kama ilivyokuwa kwa Sevilla na Getafe na
furaha yangu si kwasababu nimepata points tatu ni kwasababu DNA imerejea katika
timu yangu."
Baada ya huko nyuma
kuongea kwa mtazamo hasi kutokana na kiwango kibovu cha timu yake katika ligi ya Hispania
La Liga, jana Mourinho alikuwa mwenye furaha na kusema wachezaji wake wameonyesha
thamani zao.
"wamedhihirisha
kwangu kuwa wanaweza. Kama wanataka kuwa wachezaji wa kiwango cha juu na
uweledi mkubwa, kama wanataka kuheshimu historia ya Real Madrid, basi kila
mechi si tu dhidi ya City au Barcelona, isipokuwa kila
mchezo na wanaweza kufanya hivyo kwasababu msimu uliopita walidhihirisha hilo".
"kama
ningekuwa kocha wa timu ndogo ningeweza kupoteza mchezo mara nyingi zaidi, lakini
nikiwa kama kocha wa Real Madrid siwezi
kukubali hilo.
Nimefurahia sana
wachezaji wangu walivyofanya kwa kuwa ni ushindi mkubwa dhidi ya timu kubwa. Huo
ndio mpira wa miguu tulistahili kushinda.
Jallet: jitihada zetu zimelipwa kwa ushindi
mkubwa
Nahodha wa Paris
Saint-Germain Christophe Jallet amepongeza timu yake kwa jitihada kubwa waliyofanya
kiasi kupelekea washindi hao wa pili wa msimu uliopita katika ligi kuu ya nchini
Ufaransa Ligue 1, kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Dinamo Kiev mchezo
wa kundi A wa ligi ya mabingwa barani ulaya uliopigwa kule Parc des Princes usiku
wa jana.
Timu hiyo
toka katika jiji la Paris hii ni mara yao ya kwanza kucheza michuano ya vilabu
bingwa tangu mwaka December 2004, ambapo jana walionyesha mchezo safi na kumiliki
mchezo kiasi kipindi cha kwanza kufanikiwa kupata mabao matatu kupitia kwa Zlatan
Ibrahimovic na Thiago Silva na Alex akitumbukiza goli la tatu kabla ya
mapumziko.
Licha ya Miguel
Veloso kufanikiwa kuandika bao la kufutia machozi kwa wageni toka Ukraine , bado
Javier Pastore akaendelea kutupia bao lingine la nne na kuipeleka PSG katika uongozi wa kundi A.
Jallet amesema
kikosi chao kimesukwa vizuri na ndio maana ushindi ulikuwa rahisi lakini akiweka wazi
kuwa mchezo unaofuata wa kundi hilo dhidi FC Porto, utakuwa mgumu.
Amenukuliwa na
UEAF.com akisema
"tumetawala
kila eneo ushambuliaji na ulinzi. Jitihada zetu zimelipwa na ushindi mnono,
tumeweza kuonyesha kiwango cha michuano ya vilabu bingwa usiku huu, sasa safari
yetu kwenda Porto itakuwa kipimo kingine kigumu."
Sergio Aguero: Ningeitumikia Real Madrid wakati ule kama wangenitaka
Sergio
Aguero amesema kuwa endapo Real Madrid itaonyesha nia ya kumtaka yuko tayari
kuelekea Santiago Bernabeu, ambapo pia ameongeza kwa kusema mwaka jana 2011 alikuwa
hana chaguo lingine isipokuwa kujiunga na Manchester City.
Nyota huyo
wa kimataifa raia wa Argentina alijiunga na City akitokea Atletico Madrid majira
ya kiangazi mwaka jana kwa ada ya pauni milioni 38 na amefanikiwa kuifungia
klabu hiyo jumla ya mabao 23 katika ligi kuu ya England ikiwa ni pamoja na goli
ambalo liliipa ubingwa City katika ligi kuu ya England .
Wakati wa
kipindi cha uhamisho wake, Aguero alihusishwa kutaka kuelekea katika vilabu vingi
ikiwemo Real Madrid, lakini mchezaji huyo aliweka wazi kuwa kwa kipindi kile
hakuwa na chaguo lingine isipokuwa ni kujiunga na City licha ya Madri
kuendelea kumtaka.
Amenukuliwa baada
ya mchezo wa jana ambao City ilichapwa kwa mabao 3-2 na Real Madrid amesema
"Wakati
Madrid ikinitaka nilikuwa tayari nimeshajiunga na City na sikuwa na chaguo lingine isipokuwa kusaini
na Manchester City,"
Taarifa za kuelekea Real Madrid za Aguero zilikolezwa na vyombo vya habari lakini kipaumbele ilikuwa ni kujiunga na City, lakini pia ikaarifiwa kuwa aliogopa kujiunga na mahasimu wao wakubwa katika soka la Hispania, Atletico, kwani ingekuwa hivyp ni kuisaliti klabu yake jambo ambalo amelikanusha hakuwahi kusema hivyo.
Taarifa za kuelekea Real Madrid za Aguero zilikolezwa na vyombo vya habari lakini kipaumbele ilikuwa ni kujiunga na City, lakini pia ikaarifiwa kuwa aliogopa kujiunga na mahasimu wao wakubwa katika soka la Hispania, Atletico, kwani ingekuwa hivyp ni kuisaliti klabu yake jambo ambalo amelikanusha hakuwahi kusema hivyo.
"Sikuwahi
kusema kuwa sitaichezea Madrid kamwe kwa kuwa sitaki kuisaliti Atlético,"
Mshambuliaji
huyo kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa twitter ameandika kuwa
anajisikia furaha kuichezea City licha ya kuendelea kutakiwa na Madrid.
Ronaldo: Naweka shida chini naweka mikono juu
Cristiano
Ronaldo aliweka pembeni kwa muda huzuni na shida zake na kushangilia ushindi wa
timu yake ya Real Madrid huku mwenyewe akifunga bao la ushindi dhidi ya
Manchester City katika mchezo wa ushindi wa mabao 3-2 mchezo wa michuano ya vilabu bingwa barani
ulaya.
Mabingwa hao
wa kandanda nchini Hispania walihitaji goli la dakika za mwisho wa mchezo
kupitia kwa Karim Benzema ikiwa ni goli la kuswazisha na Ronaldo kugeuza matokeo ya kuwa nyuma kwa mabao 2-1
kuwa ushindi katika mchezo wa ufunguzi wa kundi D.
Akiongea na
TVE1 amenukuliwa
“ulikuwa
mchezo mzuri sana kwa wale walioona, tumecheza vizuri sana. Kipindi cha kwanza
kulitafuta nafasi nyingi lakini tulishindwa kuzitumia na katika kipindi cha
pili timu zote Manchester City na sisi tulicheza vizuri.
“tuliamini
tungeweza kushinda na tumefanya hivyo. Timu imefanya vizuri sana, tulijua tunaweza kufanya hivyo na tumeonyesha tunaweza.”
Mreno huyo
alipoulizwa kuhusiana na alivyoshangilia goli la ushindi hasa baada ya hivi karibuni
kunukuliwa kuwa hana furaha alijibu
“
ninashangilia pale ninapopaswa kushangilia mchezo ulikuwa muhimu na tulikuwa vitani”
.
No comments:
Post a Comment