KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, September 19, 2012

VILABU LIGI KUU VINATAKA MKATABA WA TFF NA VODACOM KUREKEBISHWA.

Wakati ligi kuu Ligi kuu Tanzania Bara ikiingia katika mzunguko wake wa pili hii leo kwa timu zote 14 kujitupa viwanjani, taarifa zilizo ifikia ROCKERSPORTS zinasema kuwa kikao kilicho itishwa na mwenyekiti wa kamati ya ligi Wallace Karia na viongozi wa vilabu kilichoketi hapo jana kimebariki kifungu kilichokuwa na utata cha EXCLUSIVITY kuondolewa na hivyo kuruhusu vilabu kutumia jezi zenye nembo ya wadhamni wao binafsi bila kujali ushindani wa kibiashara wa makampuni.
 
Sakata hilo limechukua nafasi baada ya timu ya Afrikan Lyon ya Temeka jijini Dar es Salaam kuvuliwa jezi zilizo kuwa na nembo ya mdhamini wa klabu hiyo kampuni ya simu za mikononi ya ZANTEL katika mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba mchezo uliochezwa Jumamosi iliyopita katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 Sambamba na hilo kikao hicho kimemtaka mdhamini mkuu wa ligi kuu Tanzania Bara kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom kuketi meza moja na pande zote husika kwa maana ya shirikisho la soka nchini TFF, uongozi wa vilabu na kamati ya ligi na ndani ya siku saba kutoka na majibu ya mapendekezo ya kikao chao cha  jana.

Katika kikao hicho cha vilabu pia kimemtaka mdhamini huyo kutoa vifaa na stahili nyingine za makubaliano mengine ya kimkataba ikiwemo vifaa na nauli kwa vilabu vyote 14 vinavyo shiriki ligi hiyo, kufuatia zoezi la kutiliana saini na Shirikisho la soka nchini kuwa limekwisha fanyika.

Chanzo cha  habari hii kimesema kuwa klabu iliyozua balaa hili ya Afrikan Lyon inayo milikiwa na mkurrugenzi wake Rahimu Zamunda Kangezi 'mmachinga' imekubali kuacha kutumia jezi za mdhamini wake ZANTEL mpaka mara baada ya siku hizo saba kupita ili kupisha mazingumzo hayo kufanyika na tayari wamesha muandikia barua mdhamini wake kuriadhia ombi hilo.

Afrikan Lyon imekuwa ikipinga udhamini wa Vodacoma kwa madai kuwa udhamini huo hauna fungu la kuviwezesha vilabu kumudu gharama za kuendesha vilabu msimu mzima wa ligi na kutaka TFF kusaka wadhamini wakubwa zaidi kuliko hao kama wanataka kipengele cha kuzuia ushindani wa kibiashara kuendelea kuwepo. 

Endapo hilo litafanyika hiyo maana yake ni kwamba mkataba wa TFF na Vodacom uliosainiwa bila ya vilabu kushirikishwa ambao ndio wadau wakubwa wa ligi hiyo utakuwa umefumuliwa ili kubariki kifungu hicho kuondolewa.

Wakati huo huo ligi hiyo inendelea tena hii leo ambapo wakati Simba ikiwa mgeni wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.
 
Viingilio kwa mechi ya Uwanja wa Taifa vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 wakati kwenye Uwanja wa Jamhuri itakuwa sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
 
Mechi nyingine za ligi hiyo zitakazochezwa kesho ni African Lyon vs Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Nayo Ruvu Shooting itashuka kwenye Uwanja wake wa Mabatini, Mlandizi kuikabili Mgambo Shooting kutoka Handeni mkoani Tanga.
 
Tanzania Prisons itakuwa kwenye Uwanja wake wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya kuisubiri Coastal Union ya Tanga wakati Oljoro JKT itaitembelea Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza utashuhudia mechi kati ya wenyeji Toto Africans na Azam.

No comments:

Post a Comment