KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, September 18, 2012

CITY ITASHINDA MABINGWA ANASEMA MANCINI NA WALCOTT SINTOFAHAMU ARSENAL


Mancini: City itashinda ligi ya mabingwa siku moja.
 Roberto Mancini amesisitiza kuwa siku itafika ambapo Manchester City itashinda taji la vilabu ulaya wakati huu ambapo wanaelekea kuanza kampeni ya michuano hiyo ya msimu huu dhidi ya mabingwa mara tisa Real Madrid hii leo.
City, ambayo ilitwaa taji la ligi ya England msimu uliopita itaanza msimu wake wa pili wa mafanikio barani ulaya kule Santiago Bernabeu ukiwa ni mchezo wa kundi la D linalo tazamwa kama ni kundi gumu.
Mancini anaamini kuwa klabu yake inaweza ikaendeleza mafanikio ya kutwaa mataji kama ilivyokuwa kwa mwaka 2011 walipoaanza na FA Cup na mwaka 2012 walivyo fanikiwa kutwaa Premier League na anaamini taji la vilabu bingwa litapatikana hata kama si leo.
 Amenukuliwa akisema
"kama unaendesha Ferrari unaweza kushinda tofauti na kuendesha Fiat Cinquecento, huko nyuma tulikuwa tunalifanyia kazi hili , tulizifunga timu nzuri lakini tumekuwa pamoja kwa miaka miwili na tunahitaji muda.
"nina uhakika tutafikia kushinda taji hili huko baadaye. Sijui lini lakini nina uhakika na hili. Kama tunataka kuimarika kila mwaka hili lina wezekana."
City haikufanikiwa kuvuka hatua ya makundi msimu uliopita baada ya kuwekwa kundi moja na Bayern Munich, Napoli na Villarreal.
Katika michuano ya mwaka huu itakuwa na mabingwa wa uholanzi Ajax, Ujerumani Borussia Dortmund na Hispania Real Madrid.
Ameendelea kunukuliwa akisema
"nadhan mwaka jana tulipata uzoefu, tulikuwa kwenye kundi zuri lakini haikutosha, na nadhani kundi la mwaka huu ni gumu lakini ni kundi gumu kwa kila timu.
"nadhani kilicho muhimu ni kuelekea hatua ya pili baada ya mwezi, February lolote linaweza kutokea lakini kwasasa ni ngumu kusema nini tunaweza kufanya."
 Wenger ana mashaka na hatma ya mkataba wa Walcott.
 Tukiwa tunaelekea katika michezo ya ufunguzi wa michuano ya vilabu bingwa barani ulaya , meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ameelezea juu ya hali ilivyo kuhusiana na mkataba wa wa winga wake Theo Walcott.
Hali hii inakuja baada ya wiki kadhaa za fununu kuwa katika kipindi cha dirisha la uhamisho winga huyo alikataa mpango mpya wa malipo yake ya pauni 75,000 kwa wiki na akisisitiza kutaka alipwe pauni 100,000.
 Wakati akiingia katika msimu wake wa mwisho , winga huyo mwenye umri wa miaka 23, amekuwa akimp;a homa meneja wake Arsen Wenger ambaye amekuwa akijaribu kuzima moto wa tafrani hiyo kwa lengo la kuondoa uwezekano wa kuondokewa na mchezaji huyo ikiwa ni siku chache baada ya jina kubwa la Van Persie kuondoka katika viunga vya Emirates.
Akiongea na Guardian amesema
“kwasasa bado nafikiria kumuongezea mkataba, hivyo kwa muda huu hilo halina athari kwangu.
“bila shaka kuna hatua, kama halikufanyika mwezi April unaweza ukadhani lilikuwa gumu kufanyika."
Kumekuwa na hali ya sintofahamu juu ya hatma ya Walcot kiasi kuzua maswali mengi mengi kwa mashabiki wa Arsena na sura ya winga huyo imekuwa si ya kuchangamka kama ilivyokuwa huko nyuma jambo limemfanya kupoteza kuungwa mkono na mashabiki wa klabu hiyo wanao hudhuria michezo ya Arsenal’
Amenukuliwa Wenger akisema
“ni woga tu, kila mtu anataka mchezaji wake apate  support  bila kujali hali ya mambo ya kimkataba ilivyo. Nafikiri hilo halimuathiri na pia halita athiri mashabiki wetu.
Meneja huyo wa Arsenal haja mtumia Walcott katika michezo yote minne ya msimu huu na huenda pia akafanya hivyo katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya vilabu bingwa ulaya dhidi ya Montpellier usiku wa leo.

No comments:

Post a Comment