Kocha wa Yanga Thom Saintfiet amesema amechukizwa na matokeo ya timu yake ya kufungwa na
Mtibwa sugar kwa kuwa timu yake ilikwenda Morogoro
kwa lengo la kushinda baada ya kwenda sare ya bila mabao katika mchezo
wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliopigwa katika dimba la
Sokoine mkoani Mbeya.
Amewataka
mashabiki wa Yanga wasichukie kutokana na matokeo hayo mabovu ya michezo miwili ya awali ya ligi
kwani ligi bado ndefu na yeye ameanza kufanya marekebisho ya haraka ya kiufundi ili
kupata matokeo mazuri katika mechi zinazofuata ambapo leo ameanza na kufundisha
zaidi kufunga magoli.
Akiongea na
waandishi wa habari kama kawaida yake katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko Jangwani na Twiga Kariokoo jijini Dar es Salaam, kocha huyo ameisifia Mtibwa Sugar kuwa ni timu nzuri katika kila idara, ambapo pia amesema wachezaji wa timu hiyo wana nguvu na wanacheza kinidhamu jambo ambalo linaweza kuwasaidia kumaliza ligi ikiwa katika nafasi tano za juu.
Amesema pamoja
na matokeo hayo bado ana amini Yanga watakuwa mabingwa wa ligi kuu kwa kuwa
wachezaji wake wanacheza soka la kiwango cha juu.
Thom amesema
ana imani wimbi la ushindi litaanzia katika mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu na
kuendelea hapo kesho.
Amesikitishwa
katika mazoezi ya leo asubuhi ametoa penati 6 lakini wachezaji wake wamepata
mbili jambo ambalo anasema anaomba katika michezo yao wasipate penati kwa kuwa
amekosa imani.
Amesema
katika mchezo wa kesho watakuwa wakiingia uwanjani wakiwa na hasira ya kushinda
kwani mpaka sasa Yanga ina point moja tu baada ya michezo miwili.
Ametangaza
kikosi chake kitakacho kuwa dimbani hapo kesho dhidi ya JKT kuwa Ally Mustafa
Bartez, Yaw Berko, Nadir Haroub Ally ‘Kanavaro’, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite,
Oska Joshua, Ladslaus Mbogo,Godfrey Taita, Athumani Iddi chuji, Hruna
Niyonzima, Shamte Ally, Rashid Gumbo, Stefano Mwesika, Msuva, Nizar Khalfani,
Gerson Tegete, Hamisi Kiiza, Didier Kavumbagu.
Amesema
anajua kuwa mashabiki wa Yanga wana hasira lakini hilo halimtishi yeye kama
mwalimu, kwa kuwa anafanya kazi ki-professional
No comments:
Post a Comment