KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, September 22, 2012

HAZIJATHIBTISHWA NA UONGOZI WA YANGA - NDOA NA SAINTFIET IMEVUNJIKA


Taarifa zilizo ifikia Rockersports usiku huu zinasema ndoa ya kocha raia wa Ubelgiji Thom Seintfiet na mabingwa wa kombe la Kagame Yanga imevunjika rasmi usiku huua mara baada ya kocha huyo raia wa Ubelgiji kupishana maneno na uongozi wa klabu yake ambao ndio mwajiri wake.


Sababu halisi iliyo jaa vimelea vya ukweli bado haija fahamika licha ya taarifa za kumegewa toka ndani ya kambi ya Yanga inayojiandaa na mchezo wao wa tatu dhidi ya JKT Ruvu zikisema kuwa kocha huyo aliaanza kubwata wakati akiongea na simu na kikubwa kilicho sikika ni kuwa alikuwa akilalamikia juu ya malazi yake.


Taarifa nyingine zinasema kuwa kocha huyo alikosa raha tangu aliposikia taarifa za mchana wa leo kuwa rafiki yake mkubwa John Selestine Mwesigwa ametupiwa virago na kamati ya utendaji ya klabu hiyo iliyokutana mchana wa leo katika kikao chao cha dharura.

Kibaya zaidi ni kamati ya utendaji ya klabu hiyo imempatia taarifa ya kimaandishi kumyamazisha kuongea na waandishi wa habari hata katika mambo ya kiufundi kwa madai kuwa kocha huyo amekuwa anashindwa kuheshimu utaratibu jambo ambalo limemshangaza Thom kwa kuwa hilo ni jambo ambalo liko ndani ya mamlaka yake kimkataba.


Uongozi wa Yanga mbali na kukatisha makataba wa Mwesigwa, pia umefanya kama hivyo kwa watendaji wengine kwa maana ya sekretarieti yake yote akiwemo msemaji Luis Sendeu mbali ya kuwa mkataba wake ulikuwa umemalizika tangu mwezi uliopita lakini alikuwa bado anaitumikia klabu hiyo kama msemaji.


Wengine waliotimuliwa ni aliyekuwa afisa utawala Masoud Saad, mhasibu Philip Chifuka na aliyekuwa meneja wa timu Hafidh Saleh ambaye  kazi nyingine. 


Saintfiet alianza kuuchafua uongozi wa klabu hiyo mara baada ya kurejea kutoka mkoani Mbeya ambako Yanga katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu Tanzania Bara ililazimishwa sare ya bila goli na wenyeji Tanzania Prisons mchezo uliopigwa mkoani Mbeya.

 Matokeo hayo yalimfanya kocha huyo kutoa lawama nzito kwa uongozi wa klabu kuwapeleka katika hotel ya Peter Safari ya jijini humo ambayo alidai ilikuwa na huduma mbovu za malazi na chakula pamoja na kukosa huduma muhimu ya maji. 


Katika mchezo wa pili wa ligi kuu Tanzania Yanga iliumizwa na Mtibwa Sugar kwa kupigwa mabao 3-0 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro matokeo ambayo yaliaanza kuzua maswali mengi kwa wanachama mashabiki na wadau wengine wa soka ambao walianza kuhoji juu ya uwezo wa kocha huyo licha ya kuwa na rekodi nzuri ya matokeo huko nyuma kabla ya ligi kuu kuanza.

Thom kama ilivyo kawaida yake aliwaita wana habari na kueleza kuwa hakutegemea kupata matokeo kama hayo dhidi ya Mtibwa licha ya kukiri kuwa Mtibwa ni timu nzuri lakini amejipanga kuanza ligi katika mchezo wa leo dhidi ya JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 


Itakumbukwa Yanga katika usajili wake ilifanya kufuru kwa kusajili wachezaji wake wapya kwa gharama kubwa akiwemo mlinzi Kelvin Yondani toka Simba, mshambuliaji Saidi Bahanuzi kutoka Mtibwa, mshambuliaji Didier Kavumbagu kutoka Atletico ya Burundi na Mbuyu Twite kutoka fc Lupopo ya DRC, Juma Abdul kutoka Mtibwa, Ladslaus Mbogo kutoka Toto Afrika, David Luhende kutoka Kagera Sugar, Nizar Khalfani aliyekuwa huru, Simion Msuva, Frank Domayo kutoka JKT ruvu na Ally Mustafa Bartez.


Usajili huu ulionekana kuwapendeza mashabiki wa Yanga na kunogeshwa na kocha Thom Saintfiet. 

Wachezaji hao ukichanganya na wengine wa zamani ambao hawakuachwa na timu hiyo katika usajili mpya waliwapa moyo mashabiki wa Yanga kuwa Yanga hii itajibu mapigo ya goli tano za matani wake Simba. 

Tayari minongono ilikuwepo tangu juzi jioni kuwa kocha Thom akijikwaa tu basi ataanguka na ndivyo ilivyo tokea usiku wa jana kuamkia hii leo baada ya taarifa za kuondolewa kwa Sekretarieti ya akina Mwesigwa kilicho fuata ni yeye kwani ilikuwa ni sababu tosha ya kumaliza mchezo.

tunasubiri taarifa ya uongozi wa Yanga kwa wanahabari asubuhi hii majira ya tatu kamili maana tumeitwa kuambiwa mapyaaaaaaaaaa. tukutane tena baadaye.

No comments:

Post a Comment