Bondia
wa Ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali amesaini mkataba wa kucheza
pambano la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati na Bondia Medi Sebyala wa
Uganda mchezo utakaofanyika Oktoba 14 mwaka huu katika Ukumbi wa
friends Corner.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mratibu wa mpambano huo unaosimamiwa na
Shirikisho la Ngumi za kulipwa TPBO Regina Gwae amesema mpambano huo ni
maandalizi ya kuhakikisha bondia Thomas mashali sasa anavuka mipaka ya
Tanzania baada ya kufanya vyema nchini na kwamba Bondia Medi Sebyala tayari
ameshatumiwa Mkataba wake kwa ajili ya pambano hilo.
Pambano hilo litakuwa na raundi 10 na watacheza katika uzito wa kilo
72.
Regina
amesema tunataraji pambano hilo litakuwa zuri na lenye kuvutia kwa kuwa
Mashali ni bondia mzuri na Sebyala nae ni Bondia Mzuri aliyeweka
historia ya kuwasumbua mabondia Fransis Cheka wa Morogoro na rashidi
Matumla kwa nyakati Tofauti.
Pia
amewaomba wafadhili kujitokeza kudhamini mchezo huo unatarajiwa kuwa na
mapambanio yaq utangulizi yenye kuvutia ambapo mabondia wake
waktatangazwa baadae watakaosindikiza mpambano huo.
No comments:
Post a Comment