Mabingwa watetezi
wa tali la vilabu bingwa barani ulaya wamejikuta wakipata sare ya mabao 2-2
katika dimba la nyumbani Stamford Bridge mbele ya kibibi kizee cha Turin,
Juventus.
Mshambuliaji
wa kimataifa wa Brazil akiwa katika mchezo wake wa kwanza akianza katika kikosi
cha kwanza alianza kuiandikia bao Chelsea kunako dakika ya 31 shuti ambalo lilimbabatiza
Leonardo Bonucci na kumpita mlinda mlango Gianluigi Buffon, ambaye alikuwa
akikamilisha mchezo wake wa 400 akiwa na Juve.
Mbrazil huyo
aliandika bao la pili kwa staili aina yake kufuati kupokea pasi ya Ashley Cole, na
mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21akawakwepa walinzi wawili wa Juve
kabla ya kuukwamisha mpira wavuni kwa shuti lililokwenda upande wa juu wa kona
ya goli na kuandika bao zuri.
Mabao hayo
mawili yalianza kupunguzwa na Juve dakiak tano baadaye kupitia kwa Arturo Vidal
aliyepiga mpira mzuri wa chini uliompita mlango wa mkongwe wa Petr Cech.
Zikiwa zimesalia
dakika kumi mchezo huo kumalizika Fabio Quagliarella aliyetokea katika benchi
alifanikiwa kuandika bao la kusawazisha kufuatia kuinasa pasi mbovu ya John Obi
Mikel.
Huenda Juve
wangeandika bao lingine dakika sita baadaye kufuatia Quagliarella kugeuka ndani
ya kisanduku cha hatari katika lango la Chelsea lakini shuti lake liligonga
mwamba wa goli.
Kwingineko Barcelona
ambayo ilikuwa nyuma kimatokeo ya mchezo imefanikiwa kuichapa Spartak Moscow kwa
mabao 3-2 mchezo uliopigwa Camp Nou.
Barca ndio
waliokuwa wa kwanza kuandika bao la mapema kupitia kwa Cristian Tello kabla ya Dani
Alves kujifunga mwenyewe katika harakati za kuokoa akiwa kwenye kasi kuelekea
langoni kwake kabla ya Romulo kuiandikia Spartak bao la pili kunako dakika ya 58
akifunga bao zuri akiwa katika eneo la pembeni ya lango ‘tight angle’.
Hata hivyo Lionel
Messi alifanikiwa kusawazisha bao hilo kunako dakika ya 80 na baadaye kuandika
bao la tatu kwa kichwa.
Manchester
United imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Galatasaray.
Wakiwa katika
dimba la Old Traford walifakiwa kuandika bao hilo pekee kupitia kwa Michael
Carrick kupiga mpira uliomshinda mlinda mlango Fernando Muslera lakini huenda
Galatasaray wangepata bao la kusawazisha baada ya mpira uliopigwa na Nordin
Amrabat kugonga mwamba.
United pengine
ingefanikiwa kuandika bao la pili kunako kipindi cha pili kufuatia Rafael kuangushwa
ndani ya eneo la hatari na kuamuliwa ipigwe penati ambayo ilipigwa na Luis Nani
ambayo iliokolewa na mlinda mlango Muslera.
Wao Celtic wamekwenda sare ya bila mabao na Benfica
Shakhtar
Donetsk imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya FC Nordsjaelland na kuongoza
kundi E ambalo lina timu za Chelsea na Juventus.
Henrikh Mkhitaryan ndiye
aliyekuwa mfungaji wsa mabao yote ya mabingwa hao wa zamani wa mwaka 2009 wa UEFA
Cup.
No comments:
Post a Comment