KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, September 21, 2012

NGOME BINGWA NGUMI ZA TAIFA ,MAJESHI WAENDELEA KUTAWALA NGUMI HIZO.

Michuano ya ngumi za taifa za ridhaa imefikia tamati hapo jana kwa timu ya JKT kuibuka mabingwa wa michuano hiyo iliyokuwa ikifanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

JKT imefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kufanikiwa kujikusanyia jumla ya alama 17 na kufuatiwa na Ngome iliyojikusanyia alama 13.
Nafasi ya tatu imekwenda kwa Magereza waliofanikiwa kukusanya jumla ya alama 10 wakati ambapo Polisi ikishika nafasi ya nne baada ya kukusanya alama 6.
kwa ujumla michezo hiyo ilikuwa ni mizuri na ya kuvutia kwa kuwa karibu timu zote zilionekana kujiandaa na kuonyesha upinzani mkubwa uliongoni.
Jumla ya mikoa 18 ilishirikia ngumi hizo za taifa huku timu za majeshi zikiingia kama timu na kufanikiwsa kutawala michezo hiyo kama ilivyo kawaida yao.
Mikoa iliyoshirikia ni pamoja na Ilala, Temeke, Mtwara, Pwani, Singida, Dododma, Ruvuma, Kilimanjaro, Magereza, Ngome, JKT, Arusha, Mbeya, Morogoro, Iringa.

Makore Mshaga katibu wa chama cha ngumi za Ridhaa nchini amesema amefurahishwa na michuano hiyo ilivyo fana na kukusanya watazamaji wengi waliokuwa wakishangilia kwa nguvu jambo ambalo linatia moyo chama chake.

Remmy Ngabo kocha wa timu ya Taifa ya ngumi za ridhaa amesema michuano hiyo imempa fursa nyingine ya kupata wachezaji wazuri wa timu ya taifa na tayari amefanikiwa kuwapa wachezaji zaidi ya 40 ambao anatarajia kufanya nao kazi.

Mwamuzi Juma Selemani amesema mbali na kukosa wadhambini, changamoto kubwa ni ukosefu vifaa na lakini pia angependa kuona wasichana wengi zaidi wakijitokeza katika mchezo huo.

 Hassan Mzonge kocha wa ngumi amesema bado kuna tatizo la kiufundi katika kuwajenga wachezaji hao ambao wengi walionekana kukosa mbinu zaidi za ngumi ikiwa ni pamoja ya namna ya kutembea na kujilinda jambo ambalo ameliona zaidi kwa wachezaji waliotoka mikoani.
ngumi hizo zilichezwa kuanzi kilo 42 mpaka 91.

No comments:

Post a Comment