Mshambuliaji
wa Real Madrid Karim Benzema amesema angependelea kuona anapata mafaniko
makubwa kama Zinedine Zidane.
Nyota huyo
wa kimataifa wa Ufaransa aliyejiunga na Madrid akitokea Olympique Lyonnais katika
kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2009, anatarajia kupata mafanikio kama
ilivyokuwa kwa Zidane, na mara kadhaa amekuwa akimuomba ushauri nguli huyo.
Amenukuliwa Benzema
akisema,
"nilikuwa
nikimpenda Zidane sana kwasababu na ilikuwa ndoto yangu.
Nimekutana naye na
kuongea naye. Nilikuwa nafuraha sana.
"nimekuwa
mara zote nikimuomba ushauri na alikuwa akinipa. Nategemea nitakuwa mtu tofauti
na yeye, lakini mwenye mafanikio kama yeye."
Benzema pia
ametumia fursa hiyo kumpongeza na kumsifia mshambuliaji wa zamani wa Brazil Ronaldo
De Lima ambaye alikuwa ndiye mtu wa mfano ‘Idol’.
"ulikuwa
ni msimu wangu wa kwanza katika klabu hii ya Madrid, na nilipata fursa ya
kukutana na Ronaldo,"
"nilimfuata
kama mtoto na nilivutiwa naye.
Kwangu mimi ni mchezaji mkubwa wa kipindi chote"
No comments:
Post a Comment