Ronaldo: Brazil itakuwa katika
shinikizo kubwa la kufanya vizuri kombe la dunia 2014
Mshambuliaji
nyota wa zamani wa kimataifa wa Brazil Ronaldo de Lima, anadhani kuwa kikosi cha timu ya
taifa ya nchi hiyo kitakuwa katika shinikizo kubwa la kutakiwa kufanya vizuri
wakati taifa hilo litakapo kuwa mwenyeji wa fainali ya kombe la dunia 2014, lakini
anaamini kuwa hiyo itawajengea zaidi morali wachezaji wa timu hiyo.
Ronaldo De
Lima mwenye umri wa miaka 36 alistaafu kucheza soka mwaka 2011 baada ya kufunga
jumla ya magoli 62 goals baada ya kuitumikia timu ya taifa ya Brazil ‘Selecao’
jumla ya michezo 98 lakini pia akivitumikia vilabu vikubwa duniani vikiwemo Barcelona,
Real Madrid na Inter Milan.
Amesema kutakuwa
na mengi yatakayokuwa yakitegemewa kwa wenyeji hao katika kipindi hiki cha
miaka miwili kuelekea katika fainali hiyo, huku kocha wa Brazil Mano Menezes
akiendelea kukijenga kikosi lakini anaamini kueleka kwenye michuano hiyo Brazil itaibua wachezaji
bora.
Amenukuliwa De
Lima akisema,
"najua
itakuwa ngumu kwa kikosi cha Brazil hususani katika kipindi hiki cha kuimarisha
timu"
"hakuna
shaka kuwa kucheza nyumbani kutaleta ‘pressure’ , lakini hii itakuwa ni namna
ya kujenga upya ari ya kikosi"
Katika hatua
nyingine Ronaldo amesema, mshambuliaji Neymar anaweza kuwa mchezaji mzuri zaidi
ya Messi endapo ataelekea kucheza solka barani Ulaya.
Nyota huyo
wa zamani wa vilabu vya Barcelona na Real Madrid amesisitiza kuwa wakati
mu-Argentina Messi akiendelea kung’ara duniani
kwasasa, anaamini mshambuliaji Santos Neymar ana uwezo wa kumzidi Messi.
Mourinho: Itakuwa kosa kubwa kama Ronaldo
hata shinda tuzo ya Ballon d'Or
Kocha wa Real
Madrid Jose Mourinho anadhani kuwa Cristiano Ronaldo anastahili kushinda tuzo
ya Ballon d'Or na kusema kuwa mshambuliaji huyo yuko katika kiwango kingine
ukilinganisha na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.
Mourinho amesema
baada ya mchezo mkubwa wa Clasico, wachezaji wote hao walikuwa katika sayari
nyingine lakini sasa amepata wazo jipya kuhusu kauli yake hiyo ya awali, ambapo
anaamini mshambuliaji wake Cristian Ronaldo ni bora kuliko mshambuliaji wa kimataifa wa
Argentina Lionel Messi.
Amenukuliwa akisema,
"itakuwa
ni kosa la jinai endapo Cristiano hatashinda Ballon d'Or.
Kama Messi ni bora
duniani ni kwasababu Cristiano anatokea katika sayari nyingine"
"Hajazaliwa
Madeira, lakini katika sayari ya Mars. Kwa hiyo hatokei katika sayari ya dunia.
Ndio maana ni mchezaji bora ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment