UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA DAR ES SALAAM (DRFA)
Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekamilisha
usikilizaji rufani zilizokatwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA.
Ili
kujiridhisha kuhusu uamuzi wote uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya
DRFA kuhusu waombaji uongozi wote wa DRFA waliopitishwa na ambao
hawakupitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA, Kamati itatangaza uamuzi
wake kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi wa DRFA siku ya Jumanne, Oktoba
16, 2012.
Kutokana
na hali hiyo, Uchaguzi wa DRFA uliokuwa ufanyike Oktoba 14, 2012
umeahirishwa hadi hapo uamuzi kuhusu uchaguzi huo utakapotangazwa
Jumanne, Oktoba 16, 2012.
Angetile Osiah
Katibu Mkuu
Katibu- Kamati ya Uchaguzi TFF
No comments:
Post a Comment