KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 5, 2012

RAUNDI YA SITA LIGI KUU,SIMBA VS OLJORO. YANGA VS KAGERA JUMAPILI.

Baada ya patashika nguo kuchanika katika mchezo wa vigogo wa soka hapa nchini Yanga na Simba kumalizika, michezo ya Ligi hiyo kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya sita wikiendi hii kwa mechi saba. Kesho (Oktoba 6 mwaka huu) African Lyon itakuwa mwenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
 
Nayo Ruvu Shooting itaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayochezeshwa na Oden Mbaga wa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani. Mbaga atasaidiwa na Samuel Mpenzu, Ferdinand Chacha na Andrew Shamba.
 
Jumapili (Oktoba 7 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Oljoro JKT itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar na Yanga (Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba), Mgambo Shooting na Polisi Morogoro (Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga), Toto Africans na JKT Ruvu (Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza) na Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya).
 
 

No comments:

Post a Comment