KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, August 9, 2013

JUMA NATURE, TUNDA MAN NA BINT MAJANGA SNURA KUWEKA NAKSHI MURUA SIMBA DAY TAIFA. VIIINGILIO MBONA MAJANGA.

Na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC
KESHO, Jumamosi tarehe 10 Agosti mwaka 2013, klabu ya soka ya Simba itaadhimisha kile kinachoitwa Siku ya Simba (SIMBA DAY) katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Utaratibu wa kuwa na Simba Day ulianzishwa na klabu kwa lengo la kuwa na siku ambapo wapenzi, wanachama, viongozi, wachezaji wa zamani na wa sasa pamoja na watu wengine mashuhuri, hukutana kwa pamoja na kusherehekea klabu ambayo imewafanya wawe wamoja pamoja na tofauti nyingi walizonazo.
 Mwaka huu, shughuli hiyo itafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Simba SC inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na klabu ya soka ya Sports Club Villa kutoka nchini Uganda.
 Katika kusherehesha tukio hilo, wasanii maarufu kama vile Juma Nature, Tunda Man na Snura maarufu kwa jina la ‘Mama Majanga’ watatumbuiza uwanjani hapo. Kutakuwapo pia na burudani ya muziki kutoka vikundi mbalimbali hapa nchini.
 Kabla ya mechi ya Villa, kikosi cha pili cha Simba kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya kombaini ya timu za vijana za timu za majeshi ya Tanzania kuanzia saa nane mchana. Mechi ya Villa inatarajiwa kuanza saa kumi na nusu nusu jioni.
 Milango itafunguliwa kuanzia saa sita mchana na tiketi zitauzwa hapo hapo Uwanja wa Taifa. Viingilio vitakuwa ni Sh 20,000 kwa VIP A, 15,000 kwa VIP B, Sh 10,000 kwa VIP C, Sh, 8,000 kwa viti vya rangi ya chungwa na bluu na Jukwaa la Kijani itakuwa ni Sh 5,000.
Wachezaji nyota wa Simba msimu uliopita pia watatajwa na kupewa tuzo zao. Nyote mnakaribishwa.
Maoni ya Rockersports. 
Kutokana na umuhimu wa tukio hilo la siku kubwa ya Simba ambayo ina wanachama na wapenzi wangi hapa nchini, na kwakuwa dhana nzima ya siku hiyo ya Simba ni kuwaleta pamoja wapenzi wa klabu hiyo kongwe hapa nchini kwa lengo hilo hilo lililotajwa na msemaji wa Simba Kamwaga hapo juu, na vilevile kwa kuwa ni siku ya pili ya sikukuu ya Eid fitri, ni wazi watu wengi wangependa kujumuika na familia zao wakiendeleza sherehe ya Eid basi kiingilio kingekuwa kidogo kiasi wengi waweze kumudu.
Mantiki yangu ni kwamba mapenzi ya watoto kwa klabu kubwa za Simba na Yanga hujengwa katika matukio makubwa ya kimichezo hususani wakati wanapokutana watani hawa wa soka hapa nchini.
Nadhani ingekuwa busara pia kutumia nafasi ya Simba Day kuambukiza mapenzi kwa watoto kupitia tukio kama hili, na pengine ingekuwa ni busara kuweka kiingilio kidogo ili wazazi na walezi wa watoto hao waweze kuwapeleka watoto wao kesho uwanja wa taifa na kupata faida ya kuongeza kizazi chenye mahaba na Simba.
Kiwango cha kiingilio kilichowekwa ni kikubwa mno na ambacho hakita toa uwezo kwa wazazi kwenda uwanjani na watoto wao ambao wana umri wa kati wa kutozwa kiingilio, wakati huohuo ana kabiliwa na kiingilio cha mke au mume huku pia mafuta ya gari yakimsubiri, hivyo basi fursa muhimu ya kuongeza mashabiki wa Simba inapotea.
 Mimi binafsi nilipenda moja kati ya klabu kubwa hapa nchini kwa kuhudhuria mara kwa mara uwanjani nikiwa na mzazi wangu ambaye naye ana mahaba na hiyo klabu. Nilitamani kuwa kama mchezaji fulani ambaye kila nilipo muona nilitamani kuvaa rangi ya jezi aliyokuwa akivaa pamoja na kuchora namba ya jezi yake mgongoni. 
Kumbuka mtaji wa klabu ya Simba ni wanachama.
Nawasilisha.

No comments:

Post a Comment