Gervinho amejiunga na Roma ya Italia kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 8 akitokea katika klabu ya Arsenal.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 26 alishuhudia muda wake wa kusalia ukienda kombo kwa kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza.
Alijiunga na Arsenal akitokea katika klabu ya Lille ya Ufaransa lakini katika msimu wa kwanza 2011 alifunga magoli manne tu kabla ya kufunga magoli saba katika msimu wake wa mwisho.
Taarifa ya Arsenal imesomeka
"Kila mtu angependa kumshukurua Gervinho kwa mchango wake ndani ya klabu na tunamtakia kila la kheri"
Mshambuliaji huyo aliichezea timu yake ya taifa ya Ivory Coast jumla ya michezo 45 na aliliwakilisha taifa hilo katika fainali za mataifa ya Afrika mapema mwaka huu.
Aliaanza kucheza soka katika klabu ya nyumbani ya kukuza vipaji ya ASEC Abidjan academy kabla ya kujiung na Beveren ya Belgium na baadaye Le Mans ya Ufaransa.
Alijenga jina lake katika klabu ya Lille, ambako alishinda taji la Ligue 1 na Coupe de France mwaka 2011.
Anakuwa ni mchezaji wa 13 kusajiliwa na kocha wa Roma Rudi Garcia, ambaye kikosi chake kilimaliza katika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A.
No comments:
Post a Comment