Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema kuwa biashara nzuri imefanyika katika kipindi cha uhamisho cha majira ya joto na kwamba kikosi chake sasa kimekuwa bora kukabiliana na changamoto ya michuano ya ligi kuu ya England Premier League.
Meneja huyo raia wa Chile ambaye alichukua nafasi ya kuongoza benchi la ufundi katika viunga vya Etihad mwezi Juni,
ametumia karibu kiasi cha pauni milioni £90 kwa kuwasajili wachezaji nyota wanne wakiwemo na kusema kuwa Jesus Navas, Alvaro
Negredo, Fernandinho na Stevan Jovetic na kuifanya City kuwa ni timu ya ushindi.
USAJILI WA VIKOSI VINNE NCHINI ENGLAND
Manchester City: Fernandinho (Shakhtar Donetsk, £30m), Stevan Jovetic (Fiorentina, £22m), Alvaro Negredo (Sevilla, £20m) Jesus Navas (Sevilla, £14.9m)
Chelsea: Andre Schurrle (Bayer Leverkusen, £18m), Mario van Ginkel (Vitesse Arnhem, undisclosed) Mark Schwarzer (Fulham, free)
Arsenal: Yaya Sanogo (Auxerre, free)
Wakati huo huo mshambuliaji wa Cityergio Aguero anatarajiwa kuwa fiti kuelekea kuanza kwa msimu mpya.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina alisaini kwa ada iliyoripotiwa ya pauni milioni £38 akitokea katika klabu ya Atletico Madrid mwaka 2011, anatarajiwa kurejea katika ratiba ya mazoezi wiki ijayo akikosa michezo kadhaa tangu apate kajerahaya mguu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Chelsea mwezi May.
Lakini City itakuwa ikimkosa mlinzi wake msebia Matija Nastasic katika mwezi wa kwanza wa kuanza msimu kufuatia kusumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.
Kukosekana kwake kuna maanisha kuwa mlinzi wa kimataifa wa England Joleon Lescott atakuwa akikabidhia nafasi akicheza pamoja na Vincent Kompany katika sehemu ya kati ya ulinzi.
No comments:
Post a Comment