KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, August 9, 2013

CAMEROON KUSAKA NAFASI YA KUTINGA FAINALI ZA CHAN DHIDI YA GABON HAPO KESHO.

Timu ya taifa ya Cameroon maarufu kama 'Indomitable Lions' itakuwa ikiingia uwanjani katika jaribio lao la kulinda ushindi wake wa uongozi wa bao 1-0 waliopata mjini Libreville wakati wakikamilisha mchezo wao wa pili dhidi ya Gabon, ambao ulisimamishwa kwa muda na shirikisho la soka duniani Fifa kufuatia uongozi wa kisiasa wa taifa hilo kuingilia mambo ya soka.

Mshindi wa jumla wa mchezo baina yao atakuwa akifuzu moja kwa moja katika fainali ya michuano ya wachezaji wa ndani CHAN fainali ambazo zitapigwa nchini Afrika kusini kuanzia January 11mpaka February mosi wakati ambapo atakayefungwa atapata nafasi ya kucheza mchezo wa kapu la bahati play-off dhidi ya Democratic Republic of Congo.

Kutakuwa pia na michezo mingine ya mkondo wa pili na mchezo wa mkondo wa kwanza mwishoni mwa juma hili ambapo Zimbabwe watakuwa wakiwakaribisha Zambia mjini Harare na Mozambique watakuwa wakiwakaribisha Angola mjini Maputo.
 
Burkina Faso, Burundi, Congo Brazzaville, Ethiopia, Ghana, Libya, Mali, Mauritania, Morocco, Nigeria na Uganda tayari zimesha fuvu kuelekea katika fainali hizo nchini Afrika kusini.

No comments:

Post a Comment