Aly Cissokho (kulia)
Mlinzi wa Valencia Aly Cissokho ameweka wazi kuwa amekubaliana na Liverpool juu ya maslahi yake binafsi kuelekea katika mpango wake wa kuelekea Anfiled.
Bosi wa wekundu hao Brendan Rodgers amekuwa akifukuzia saini ya mlinzi huyo wa kushoto karibu kipindi chote cha kiangazi ambapo kabla ya hapo alikuwa akiitaka saini ya mlinzi wa Chlesea Ryan Bertrand.
Lakini licha ya taarifa kuenea nchini Hispania kuwa Liverpool ilikuwa ikimtaka mlinzi wa Granada Guilherme Siqueira inavyoonekana ni kwamba Cissokho atakuwa ndiye sahihi kuelekea Anfield, licha ya kwamba mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 25 kusema kuwa bado kuna mambo kadhaa ya ndani yanazungumzwa baina ya pande hizo mbili
No comments:
Post a Comment