msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga |
Klabu ya smba imesema inasikitishwa na jinsi shirikisho la
soka nchini TFF linavyo jitahidi kuhakikisha Simba haipati haki yake kwa kuwa
mpaka sasa Yanga haijalipa pesa za mbuyu Twite.
Akiongea na waandishi wa habari hii leo msemaji wa klabu Ezekiel Kamwaga amesema Simba imeliandikia barua shirikisho hilo ili liwapatie
maamuzi ya kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji inaongozwa na
mwanasheria Alex mgongolwa iliyokutana hivi karibuni kuamua kesi mbalimbali zinazo husu matatizo ya usajili kwa msimu wa 2012/2013 .
Mpaka sasa Simba haijakabidhiwa taarifa ya maamuzi ya kamati
ya Mgongolwa kuhusu suala la mlinzi wa Yanga Mbuyu Twite jambo ambalo Simba
inaona TFF haitendei haki.
Aidha msemaji huyo amesema Simba katika mchezo wa kesho imeomba kupatiwa pesa za
mgao wao palepale uwanjani baada ya mchezo na Yanga kumalizika.
Sambamba na hilo Saimba imemtaka mwamuzi aliyepewa dhamani
ya kuchezesha mchezo huo wa kesho Methew Akrama
wa Mwanza ambaye ndiye alikuwa mwamuzi katika mchezo wa Yanga dhidi ya Lyon
achezeshe kwa kufuata kanuni na sheria 17 za mchezo wa soka hiyo kesho na kutoa tafsiri
sahihi ya sheria.
Simba wamemtaka mwamuzi huo kufanya hivyo kwani ataokoa
maisha ya watu.
Klabu hiyo kongwe ya Simba imesema wanajua kuwa katika mchezo huo alikuwa amepagwa mwamuzi mwingine lakini amebadilishwa ili
achezeshe yeye kwa kuwa mchezo utakuwa unaonyeshwa moja kwa moja na kituo
kikubwa cha television cha Supersport kwa kuamini kuwa atachezesha vizuri na
kujitengenezea jina lake duniani.
Aidha Simba imeshangazwa na kitendo cha kuitaka Simba kuiandikia
barua Yanga wawagawie pesa zao katika mapato yatakayo patikana katika mchezo wa
kesho ilihali TFF ilitoa siku ishirini na moja ili Yanga wawe wameilipa Simba
na kesho ndio mwisho.
No comments:
Post a Comment