Wazee wa klabu ya Yanga wameunda kamati maalum
inayoshirikisha mikoa 20 ya Tanzania Bara kwa ajili ya kusimamia ligi nzima na
kwa kuanzia wanaanza na mchezo wa kesho dhidi ya watani wao wakubwa katika soka
la Tanzania Simba.
Akiongea na waandishi wa habari msemaji wa wazee hao Abdalah
Mohamed Kibavu amewataka mashabiki wa
Yanga kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa hiyo kesho kushuhudia jinsi mnyama
atakavyokuwa akiuwawa.
Kabla ya hii leo mzee Kibavu kuongea na waandishi wa habari, juzi mara baada ya mkutano wao na mwenyekiti wao Yusufu Manji mzee mwingine maarufu Yusufu Mzimba akiongea na Rockersports alisema wameamua
kuungana kwa lengo la kukusanya nguvu ya pamoja na viongozi
wao wa juu wa Yanga ili kutoa msaada na uzoefu wao katika kufanikisha
azma ya ushindi.
Amesema kinacho wasukuma zaidi ni
kutokana na dhamira ya kweli ya ushindi kutoka kwa mwenyekiti wao Yusufu
Manji akishirikiana na viongozi wengine wa kamati ya utendaji ambao
kimsingi wameomba msaada kutoka kwao ili kufanikisha ushindi mnono
utakao wafariji wana Yanga ambao bado wanaumizwa na kichapo cha mabao
5-0 cha mchezo uliopita.
Mzee Mzimba amesema yeye kama walivyo
wanachama na wapenzi wengine wa Yanga bado wana kumbukumbu mbaya ya
kichapo cha mabao 5 ambayo amesema yalitokana na uongozi uliomeguka wa
Lyod Nchunga ambao ulikosa umoja na kupenyezwa hujuma za makusudi ili
kuidhalilisha klabu yao.
Aidha amesema watajitahidi kwa kadri
itakavyo wezekana wao kama wazee wa klabu kwa kushirikiana na uongozi wa
klabu wakiongozwa na Manji, viongozi wa matawi na mikoa pamoja na kundi
la vijana wa klabu hiyo kuhakikisha mnyama anauwawa jumatano hata kama
si kwa idadi ya mabao 5 basi yasipungue mabao 3.
No comments:
Post a Comment