Shirikisho la soka nchini TFF limewataka mashabiki wa soka
wajitokeze kwa wingi katika uwanja wa Taifa kesho kungalia mchezo mkubwa wa
soka kati mabingwa watetezi wa ligi ya soka Tanzania bara Saimba dhidi ya
mahasimu wao wakubwa kisoka Yanga, mchezo ambao utapigwa hapo kesho katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akiongea hii leo katibu wa shirikisho hilo Angetile Oseah 'ngeta' amewataka mashabiki kuwa na nidhamu na
kuimarisha hali ya usalama na hatimaye kurejea majumbani salama ikiwa ni mchezo
ambao unahitimisha super wiki ya supersport.
Mchezo huo umepangwa kufanyika
usiku kuanzia saa moja kamili.
Wakati huohuo, TFF kwa kushirikiana na kampuni ya Prime
Time Promotion wameamua kuanzisha soka la ufukweni huku TFF ikijipanga kuunda
kamati itakayoshughulikia mchezo huo.
Wao Prime time Promotio watakuwa na jukumu la kuutangaza
mchezo huo kwa maana ya Promotion mchezo ambao umepangwa kuzinduliwa mwezi wa
desemba baada ya mafunzo kutolewa na wakufunzi
kutoka shirikisho la soka duniani FIFA mafunzo ambayo yanatarajiwa
kutolewa mwezi wa Novemba na kwa kuanzia wataanzia na fukwe za Dar es Salaam na
uzinduzi ukitarajiwa kufanyika katika ufukwe wa Coco beach.
No comments:
Post a Comment