Meneja wa
Arsenal, Arsene Wenger amesema kumpoteza Abou Diaby kutokana na majeraha
aliyoyapata ni pigo kubwa.
Kiungo huyo
mfararansa huyo alipatwa na matatizo ya msuli wa paja katika mchezo ambao timu
yake ilipokea kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Chelsea.
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 26 alikuwa katika kiwango safi msimu huu baada ya kukosekana
kwa muda mrefu lakini sasa kutokana na majeraha aliyopata bila shaka atakuwa
nje ya uwanja si chini ya wiki tatu.
Arsene Wenger
anaamini Diaby alikuwa vizuri katika mchezo dhidi ya kikosi cha Roberto Di
Matteo, na anaamini kikosi kingeibika na ushindi katika mchezo huo.
Amenukuliwa
akisema,
"kumpoteza
Diaby ni pigo kubwa, ndio. Si tu kwasababu tumepoteza mchezaji mzuri lakini
alikuwa na ubora ambao wachezaji wengine hawana.
"kwa
mfano jumamosi alipotoka na nafasi yake kuchukuliwa na Alex Oxlade-Chamberlain,
tulikuwa tunapoteza mipira mingi.
"ilikuwa
ni mipira ambayo Diaby angekuwa anaicheza kwasababu anaweza, ni mchezaji mwenye
nguvu.
"kwa
kweli inachanganya sana kwani ukipanga hivi linatokea lingine."
Licha ya
kuwa na pengo hilo la sehemu ya kiungo, Wenger amewataja viungo wengine katika
kikosi chake kuwa wataweza kufanya kazi iliyoachwa na Diaby.
Ameongeza
kwa kusema,
"tunaye
Aaron Ramsey, Francis Coquelin, Alex Oxlade-Chamberlain na Jack Wilshere. Itategemea
kama tunataka kulinda zaidi ama la.
"Arteta
anaweza kucheza sehemu ya mbele “higher and deeper” . Hivyo tunaweza
kumuingiza mchezaji wa aina hiyo kama Coquelin na pia Arteta wanaweza kusukuma
mipira mbele."
No comments:
Post a Comment