Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amejitapa kuwa
washambuliaji wake Wayne Rooney na Robin van Persie ndio washambuliaji wakali
kwa sasa baada ya kuunganisha nguvu zao na kuchomoza na ushindi dhidi ya CFR Cluj ya Romania, mchezo
wa ligi ya mabingwa ulaya ulichezwa usiku wa kumkia leo.
Meneja huyo
mkongwe mwenye umri wa miaka 70 alikuwa akiangalia namna vijana wake
walivyofanikiwa kudhoofisha kikosi cha CFR Cluj ya Romania ambacho kilipata bao
la uongozi kupitia kwa Pantelis Kapetanos kwa goli la mapema na la kushtukiza.
Hata hivyo
United ilirudi mchezoni huku Rooney akitoa pasi za mwisho mara mbili kwa Van
Persie na kuhakikisha United ikiondoka pande za Transylvania ikiwa na points zote tatu
muhimu katika kipindi ambacho mashetani wekundu wakionekana wakiwa na matatizo
katika sehemu ya kiungo na ulinzi lakini ushambuliaji wakiwa wanatisha.
Akinukuliwa na
kituo cha television cha ITV amesema,
"ubora
wa kikosi uko mbele ITV, wanapasiana na wanafunga wote walikuwa vizuri. Ni umaliziaji
mzuri na ule ulikuwa mpira mzuri Wayne kamdondoshea Persie. Nadhani ulikuwa
mpira mzuri."
Hata hivyo Sir
Alex amekataa kusema kama hiyo ndio wachezaji wake pacha katika sehemu ya
ushambuliaji na badala yake amesema katika kikosi chake kunawachezaji wengi
wakubadilishana kucheza.
No comments:
Post a Comment