Meneja wa AC
Milan Massimiliano Allegri anaamini kikosi chake kina kila sababu ya kuimarika
zaidi katika kipindi hiki wakiwa wanaelekea katika mchezo wa ligi ya mabingwa
Ulaya usiku huu dhidi Zenit St Petersburg.
Milan ambao
wako katika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi ya soka ya Italia maarufu kama ‘Serie
A’, meneja wake ambaye yuko katika shinikizo kubwa la matokeo mabaya, anadhani vijana
wake wanatakiwa kufanya jitihada zaidi ili kuwaadhoofisha wapinzani wao.
Amenukuliwa akisema,
"tunapaswa
kudhihirisha kuwa tunatimu nzuri yenye ufundi mkubwa. Lakini pia bado kuna
mengi ya kujifunza ili kuimarika zaidi".
"Zenit ni
timu nzuri. Soka la Urusi ni kubwa. Uwepo wa Hulk na Axel Witsel imeonyesha
kuwa kuwa wamepiga hatua kubwa mbele.
"Luciano
Spalletti ni kocha mzuri. Ameshinda Coppa Italia akiwa na kikosi cha Roma, na ameshinda
ligi hapa Urusi. Timu zake mara nyingi huwa zinacheza soka zuri."
Wakati huohuo
mmiliki wa Milan Silvio Berlusconi amekanusha taarifa za fununu kuwa alikuwa
anafikiria kufanya mabadiliko katika nafasi ya makamu wa Rais inayoshikiliwa na
Adriano Galliani kutokana na matokeo mabovu ya timu yake.
Amenukuliwa akisema,
"natumia
fursa hii kukanusha taarifa hizo, na ninaweka wazi juu ya ninavyo mkubali na
nilivyo na imani na Adriano Galliani, kumekuwepo na baadhi ya taarifa kuhusiana
na Milan hizi taarifa ziko mbali na ukweli.
"ni
mmoja kati ya watu muhimu katika mchezo, na ni rafiki yangu kwa zaidi ya miaka 30
nina muheshimu sana."
No comments:
Post a Comment