Mlinzi wa Manchester
City Pablo Zabaleta ametoa maneno ya utani akisema kuna wakati inatokea
unatamani kumuua Mario Balotelli kutokana na tabia za ajabu
ajabu za mshambuliaji huyo.
Amenukuliwa Omnisport
Zabaleta akisema
"ukiwa
mchezaji wakati mwingine si kila ulicho nacho mguuni ndicho kilichopo kichwani
na Mario anatabia hiyo, huyu mwenzetu unaweza ukacheka kwa yale anayofanya na
wakati mwingine ukatamani hata kumuua, lakini mwisho wa siku ni mzuri tu".
Zabaleta ameongeza
kwa kusema tangu kuwasili kwake Manchester amekuwa gumzo, lakini licha ya
matatizo yake mshambuliaji huyu ni mwenye malengo makubwa.
Mlinzi huyo
mwenye umri wa miaka 27 anaamini mchezaji mwenzi wake huyo anaweza kufika mbali
katika soka na kupata tuzo ya heshima na
kwamba yuko katika klabu ya kweli na meneja anaye weza kufika huko.
"tangu
kuwasili kwa Mario amekuwa na mambo mengine ya sawa na wakati mwingine ya
hovyo, kama mchezaji ni mchezaji mwenye kipaji.
Kama atataka kupigania tuzo ya Ballon d’Or kama ilivyo kwa Messi na Cristiano
Ronaldo anaweza kufanya hivyo ingawa hatashinda lakini anaweza kuwa karibu
nao na kuwa mshambuliaji mkali duniani.
Torres: Chelsea ndio wenye nafasi ya kutwaa kombe la dunia la vilabu.
Mshambuliaji
wa Chelsea Fernando Torres anaamini kuwa timu ndio yenye uwezo wa kutwaa taji
la michuano ya vilabu bingwa duniani, ambapo amesema kushinda taji hilo ni lengo
kubwa msimu huu.
Amenukuliwa na
FIFA.com akisema
“Chelsea ndio yenye nafasi ya kushinda taji hilo lakini
kwangu kuwa kwenye nafasi ya kufanya hivyo si kitu”.
“kitu pekee
cha kufanya ni kuongeza morali na juhudi, na mwisho wa siku haijalishi kuwa mwenye nafasi
ya kushinda ama laa, unapaswa kudhihirisha hilo uwanjani"
Klabu hiyo
yenye maskani yake kaskazini mwa jiji la London itaingia katika michuano hiyo
mwisho wa mwezi huu ikiwa ni baada ya kutwaa taji la vilabu bingwa Ulaya taji
ambalo walilitwaa mwezi May, na Torres anasema maandalizi ya michuano hiyo
itakuwa imekamilika.
No comments:
Post a Comment