Neymar da Silva Santos Júnior si
mdogo kuibeba wa kushindwa kubeba matumaini ya Brazil kushinda kombe la dunia. Hii ni kauli ya kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari.
Mshambuliaji
huyo wa klabu ya Santos ambaye kwasasa ana umri wa miaka 20, amekuwa akitazamwa
na baadhi ya watu kama bado kinda kuweza kubebeshwa matumaini ya Brazil, lakini Scolari
ana matumaini kuwa uwezo wa mchezaji huyo ni chachu ya mafanikio wakati Brazil
itakapokuwa mwenyeji wa michuano mikubwa ya kombe la dunia 2014.
Scolari ametolea mfano kwa mkongwe Edison Arantes do Nascimento 'Pele', kuwa alikuwa
kijana mdogo wakati nchi hiyo ilipochukua taji mwaka 1958, kama ilivyokuwa kwa Ronaldo Luís Nazário de Lima.
Alipoulizwa
juu ya umri Neymar na matumaini ya mchezaji huyo kwenye kikosi amesema mbona Ronaldo
alitumiwa kuiongoza Seleção, na alifanya hivyo akiwa na umri wa miaka 19 na 20.
"Pele
pia alikuwa na umri wa miaka 17 tu , licha ya kwamba hakuwa na jina kubwa
wakati huo na alifanikiwa kutengeneza jina wakati na baada ya kombe la dunia 1958.
Man United
waonywa kuachana na mpango wa Lewandowski.
Matumaini ya
Manchester United kumsajili Robert Lewandowski katika usajili wa mwezi januari
yameanza kutiwa mashaka baada ya klabu yake ya Borussia Dortmund kuthibitisha
kuwa mshambuliaji huyo atasalia Bundesliga.
Lewandowski
mwenye umri wa miaka 24, amekuwa akihusishwa kuelekea katika ligi kuu ya nchini
England “Premier League” katika klabu ya Manchester.
Bosi wa Dortmund
Jurgen Klopp amesisitiza kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Poland bado
hajatoa ombi la kutaka kuondoka nchini Ujerumani licha ya kwamba mpango huo uko
ndani ya maamuzi yake.
Akikaririwa Klopp
amesema
"sina
wasiwasi kuwa ataondoka, Manchester United ni moja miongoni mwa timu sinazo
mkodolea macho lakini ukweli ni kwamba atasalia na sisi.
"Ahsante
mungu, wakati wa klabu kubwa tajiri ya England kujaribu kuchukua wachezaji wetu
sasa umekwisha. Wakati wa mzunguko wa pili wa msimu ataendelea kukaa nasi"
Klopp anaamini
kuwa Bundesliga kwasasa ni ligi kubwa kuliko Premier League, licha ya kwamba Shinji
Kagawa aliondoka Dortmund kiangazi.
Mabingwa hao
wa ujerumani hii leo watakuwa wenyeji wa Manchester City katika mchezo wa
vilabu bingwa Ulaya ambapo licha ya kuwa tayari klabu hiyo imeshapata nafasi
katika hatua ya mtoano, Klopp atashusha kikosi cha nguvu kusaka uongozi wa
kundi D.
No comments:
Post a Comment