KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, November 1, 2012

COAST UNION YATEPETESHWA NA AZAM FC CHAMAZI. YAGONGWA 4-1.



Azam fc chini ya kocha wake Stewart John Hall hii leo imefanikiwa imerejesha cheche zake katika mbio za kuwania taji la ligi kuu Tanzania bara baada ya kufanikiwa kuichapa Coast Union ya Tanga jumla ya mabao 4-1, katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex ulioko Mbande nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam.
Bao la kwanza la timu hiyo liliwekwa kimiani na mshambuliaji mrefu Gaudience Mwaikimba kabla ya Kipre Tcheche kuandika bao la pili katika kipindi cha kwanza huku bao la Tatu likifungwa na Hamisi Mcha 'Viali'.
Hadi mapumziko Azam 3 Coast Union 0.

Kipindi cha pili Azam ilifanikiwa kuandika bao la nne kupitia kwa Hamisi Mcha tena kabla ya Jerry Santo kuiandikia Coast Union bao la kufuatia machozi.

Coast Union hii leo hawakuwa katika kiwango kizuri tangu kuanza kwa mchezo licha ya wakati fulani timu hiyo kuonekana kujaribu kutulia na kufanya mashambulizi ambayo ambayo hayakuwa na malengo na kuwafanya walinzi wa Azam wakiongozwa na nahodha Aggrey Moris akisaidiwa na Saidi Moradi sehemu ya kati kuokota mipira mingi inayokufa kutoka kwa washambuliaji wa Coastal.

Matokeo hayo yameifanya Azam kufikisha jumla ya alama 21 na katika mchezo ujao wakitarajiwa kukutana na Yanga Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment