KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 2, 2012

Neymar: kucheza timu moja na Messi itakuwa ndoto,Ronaldinho anusurika katika ajali na Mouronho: sijui nitakuwa wapi baada ya Real Madrid..

Neymar: kucheza timu moja na Messi itakuwa ndoto.
Mshambuliaji wa Santos ya nchini Brazil Neymar, ameweka wazi kuwa itakuwa ndoto yeye kucheza akiwa pamoja na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.

Mbrazil huyo kwa kipindi kirefu alikuwa akihusishwa kutaka kuelekea Camp Nou, na hivi karibuni Peixe alikaririwa akisema mpango wa uhamisho ulikuwa tayari kwa kijana huyo kuelekea kwa kigogo hicho cha Catalunya.

Hata hivyo mshambuliaji huyo mbichi na mwenye uwezo mkubwa akiwa na umri wa miaka 20 kwa mara nyingine ameondosha matumaini hayo na kwamba kikosi cha Tito Vilanova kinaweza kuwepo katika fikra zake endapo ataamua kuachana na soka la Marekani ya kusini.

Amenukuliwa na gazeti la Marca akisema,
"kucheza na Messi itakuwa ndoto. Labda kufanya na ye mazoezi hiyo nitafurahia sana,".

Mshambuliaji huyo kijana anaamini kwamba wakati  Cristiano Ronaldo na Andres Iniesta wakiwa katika kiwango cha juu na wachezaji wakubwa duniani kwasasa lakini anaamini kuwa hakuna anayestahili tuzo ya Ballon d'Or zaidi ya Messi.

"kwa upande wangu kuna wachezaji watatu ambao ni wazuri sana kuliko wengine, Iniesta, Ronaldo and Messi," "lakini Messi ndiye bora. Hakuna mtu anayeweza kufanya vitu anavyo fanya."

Neymar pia amemshukuru Messi ambaye mtaja yeye kuwa ndiye atakaye fuatia kuchukua tuzo hiyo kwa kusema ni mchezaji mzuri "excellent footballer".

"unadhani mchezaji kukusifia? Imenifurahisha namshukuru kwa maneno yake".

Ronaldinho anusurika katika ajali.

Nyota wa Atletico Mineiro Ronaldinho amenusurika katika ajali ambayo ilihusisha magari matatu.

Wakati ajali hiyo ikitokea kiungo huyo wa zamani wa Barcelona alikuwa akiendesha gari kuelekea katika uwanja wa mazoezi ya timu yake.

Mbrazil huyo alinusurika kufa katika ajali hiyo kufuatia gari lake kukwepa wakati ambapo mmoja kati ya medereva wa ajali hiyo alikimbizwa katika chumba cha unagalizi wa dharura baada ya kugongana.

Gari ambalo lilihusika moja kwa moja na ajali hiyo liliharibika vibaya lakini abiria wamenusurika.

Mchezaji mwenzake Jo aliyepita katika eneo la ajali hiyo la Lagoa Santa, alithibitisha kuwa Ronaldinho alipona na kwamba alifika katika uwanja wa mazoezi ndani ya muda muafaka.

Mchezaji huyo bora wa dunia wa zamani ambaye yuko katika kiwango cha juu katika klabu ya Atletico akiwa amekwisha kufunga magoli saba msimu huu, anatarajiwa kuwepo dimbani jumapili katika mchezo wa ugenini dhidi ya Coritiba.

Mouronho: sijui nitakuwa wapi baada ya Real Madrid.

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amesema kuwa bado hajajua muelekeo wake baada ya kuondoka katika klabu hiyo.

Baada ya kushinda taji la ligi kuu ya nchini Hispania akiwa Los Blancos, mreno huyo amekuwa kocha wa kwanza katika historia kushinda mataji makubwa ya ligi za ndani katika nchi za Italia, England na Hispania.

Mourinho ameweka wazi njaa yake ya kutaka kuendeleza mafanikio katika soka.

Amenukuliwa na jarida la Ronda Ibera akisema,
"tangu nikiwa mdogo nilijua kuwa ili kuendelea katika kazi yangu ni lazima nitembee katika mataifa mengine. Nilijua nahitaji kusafiri, kukutana na changamoto mpya ili niweze kukuwa"

"nilipo anza kusafiri , dhamiri yangu ilikuwa katika mataifa ya England, Italia na Hispania. Nitakapo ondoka hapa Real Madrid, sijui nitaelekea nielekee wapi katika kazi yangu.

"bado najipigania, siku zote nataka kufanya vizuri. Hivyo basi nafikiria wengine na hilo linanisaidia.

"ugumu wa kufundisha unaongezeka siku hizi. Kocha wa leo hawezi kuwa katika uwezo ule ule kama ilivyo miaka 10, 20 au 30 iliyopita.

"ugumu wa kocha unakuwa katika kuchagua wachezaji 11, kufundisha mbinu na kufanya mabadiliko."

Mourinho pia akazungumzia jinsi ambavyo soka linavyo athiri maisha yake ya kawaida akuzungumzia juu ya namna anavyo jitoa katika kufikia mafanikio.

"mtoto wangu hawezi kwenda chuo bila wengine kumjua yeye ni nani. Mke wangu anataka nibakie ndani ya gari wakati akiingia madukani kufanya ‘shopping’.

"hii inanigharimu katika kufanikisha uweledi katika kazi yangu ninayo ipenda. Nimekuwa nikihusika na soka tangu nimezaliwa. Sasa nakaribia miaka 50 umri ambao una maana kubwa.

No comments:

Post a Comment