KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 6, 2012

HABARI ZA AZAM KUMUUZA NGASA EL MERREKH, ALHAJI ISMAILI ADEN RAGE AWAPA SIKU SABA KUTHIBITISHA TUHUMA ZA RUSHWA KWA VIONGOZI WA SIMBA. ASEMA WAMECHOKA KEJELI ZAO. ANASEMA NGASA HANG'OKI WANAJIFURAHISHA

Mwenyekiti wa mabingwa wa soka nchini Simba ya jijini Dar es Salaam Alhaji Ismail Aden Rage amesema klabu ya Azam inayoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania Bara itakuwa inajifurahisha tu endapo ni kweli itakuwa imekamilisha taratibu za kumuuza mshambuliaji Mrisho Ngasa kuelekea katika klabu ya El Merreck ya Sudani.
Kauli ya Rage inafuatia kuwepo na taarifa iliyochapishwa hii leo katika Tovuti ya klabu hiyo kuwa klabu hiyo imekamilisha taratibu za kumuuza Ngasa kuelekea El Merreikh ya Sudani.

Taarifa hiyo imesomeka kwa kichwa cha habari "Ngasa atua Ell Mereikh kwa $75,000"

Kwa mujibu wa maelezo ya kina ya tovuti ya Azam ni kwamba
Azam FC leo imemuuza mchezaji wake Mrisho Halfan Ngasa kwa klabu ya El Mereikh katika majadiliano  yaliyochukua takriban saa moja kwenye makao makuu ya klabu ya Azam FC na kuhudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili.

El-Mereik wameshazungumza na mchezaji na kukubaliana maslahi yake binafsi ambapo Mrisho Ngasa atalazimika kusafiri hadi mjini Khartoom Sudan mara baada ya kuisha mashindano ya CECAFA Challenge Cup ili kuona mazingira ya klabu, kufanya vipimo vya Afya na kuangalia makazi yake binafsi.

Kuuzwa kwa Mrisho Ngasa nchini Sudan kunaifanya klabu ya Azam FC kupata kiasi cha zaidi ya Dola 50,000 pesa ambayo Azam FC waliiweka kama kima cha chini cha kumuuza Mrisho Ngasa.
Wakati Azam FC ikimtoa Ngasa iliweka kiasi hicho cha dola 50,000 kwa timu itakayomtaka lakini kutokana na kukosekana na mnunuzi huku Simba ikitoa ofa ya shilingi milioni 25, Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo ili akitokea mteja mwenye kufikia dau hilo waweze kumuuza.

  Pia taarifa hiyo imeongeza kwa maneno kuwa,
"Mengi yalisemwa juu ya biashara ya mkopo kati ya Azam FC na Simba lakini msimamo wa Azam FC uliowekwa kwenye tovuti hii leo umethibitika baada ya El-Mereikh kufikia dau la kumnunua Mrisho Ngasa".

"Mrisho Ngasa, mchezaji mwenye kipaji cha hali ya Juu cha kusakata kabumbu anakwenda nchini Sudan kwenye kikosi chenye mafanikio zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati baada ya TP Mazembe".
.
 Akiongea na Rockersports Mwenyekiti wa Simba Alhaji Rage amesema watanzania wanapaswa kuwa waangalifu na taarifa za mitandaoni kwani zinaweza kupotosha mambo.

Rage amesema mshambuliaji huyo alikopeshwa Simba kwa maandishi ambapo pia Azam ilipewa shilingi milioni 25 kwa makubaliano pia Simba kumlipa mshahara na gharama nyingine kama nyumba na gari.

Amesema ni kweli Simba hairuhusiwi kumuuza kwenda klabu nyingine hadi muda wake wa mkopo utakapo malizika Simba.

Rage amewataka Azam ndani ya Siku saba kuthibitisha tuhuma za rushwa kwa viongozi wa Simba ambapo Azam iliituhumu Simba kutoa rushwa wachezaji wao ili kupanga matokeo katika mchezo uliozikutanisha timu hizo katika ligi kuu.

BOFYA HAPA KUMSIKILIZA.
  

No comments:

Post a Comment