Mshambuliaji
nyota wa Barcelona Lionel Messi amejikuta akitolewa nje kwa machela kutokana na
kupata maumivu makali katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Benfica.
Tito
Vilanova hakumuanzisha mshambuliaji huyo kama ilivyo kawaida yake na kumuingiza
katikati ya mchezo kipindi cha pili kwa lengo la kusukuma mashambuliaji zaidi.
Zikiwa zimesalia
dakika tano mchezo huo kumalizika wakati huo matokeo yakiwa ni sare ya bila
mabao, mshambuliaji huyo anayetazamiwa na wengi kushinda tuzo ya Ballon d'Or
favorite aliwekwa chini na kuanza kulalamikia maumivu ya mguu wake kabla ya
kutolewa nje ya dimba la Camp Nou kwa matibabu.
Maafisa wa
Barcelona muda mfupi baadaye wakatumia mtandao wa kijamii wa twitter kwa kutoa
ujumbe
"Messi
amepatwa na mchubuko katika mguu wake wa kushoto . Anatakiwa kufanyiwa vipimo
zaidi ukubwa wa jeraha lake,".
Baada ya
mshambuliaji huyo kutolewa nje hakukuwa na mabadiliko yoyote ya matokeo na
hivyo mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 0-0, matokeo ambayo yanaiondoa Benfica
mashindano na kusogezwa katika Europa League wakati ambapo Celtic ikisonga mbele
baada ya kuichapa Spartak Moscow.
Wengi walitazama
kuwa usiku wa jumatano hii utakuwa ni usiku wa kihistoria kwa Messi kuvunja
rekodi ya Gerd Muller ya kufunga magoli 85 katika kipindi cha mwaka mmoja.
Aidha majeraha
ya Messi huenda yakamuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki kadhaa mpaka
katika kipindi cha majira ya baridi, hiyo ikimaanisha kuwa Messi atakuwa
ameshindwa kuvunja rekodi hiyo ya mwasisi wa kijerumani Muller.
No comments:
Post a Comment