Robo
Fainali za michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana
wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zitachezwa
kesho (Desemba 19 mwaka huu) kwenye viwanja vya Karume na Chamazi jijini
Dar es Salaam.
Mtibwa
Sugar itaumana na African Lyon kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
katika mechi itakayoanza saa 2 kamili asubuhi. Nazo Azam na JKT Ruvu
zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 2 kamili asubuhi.
Mechi
nyingine ya robo fainali itakuwa kati ya JKT Oljoro na Simba ambayo
itachezwa kuanzia saa 9 kamili alasiri kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume. Coastal Union na Ruvu Shooting zitacheza kwenye Uwanja wa
Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nusu
fainali ya michuano hiyo itachezwa Ijumaa ya Desemba 21 mwaka huu
Uwanja wa Chamazi, wakati fainali na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu
zitapigwa Jumapili ya Desemba 23 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume.
No comments:
Post a Comment