KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 15, 2012

BIASHARA: MANCHESTER CITY YATANGAZA HASARA KWA MWAKA WA PILI MFULULIZO.


Manchester City imetangaza hasara ya euro million 120 kwa mwaka wa fedha ulio malizikia May 2012, licha ya kwamba hasara hiyo ni pungufu ukilinganisha na euro milioni 243 iliyotajwa miezi 12 ya nyuma.
 Manchester City imetangaz hasara hiyo ambayo ni mwaka wa pili mfululizo ambapo klabu hiyo tajiri ilipoteza euro milioni 120 katika kipindi cha mwaka mwaka wa fedha wa nyuma ya hapo kwa maana ya 2010/2011.


Licha ya kukusanya euro milioni 283 katika kipindi cha mwaka huo wa 2011/2012 ambacho kimsingi ni kikubwa katika historia ya klabu hiyo, kiasi ambacho kimepanda kutoka euro milioni 184 mwaka uliopita, lakini bado ukilingana na matumizi ya msingi ya uendeshaji ya klabu ndani ya kipindi hicho klabu hiyo imejikuta ikipata hasara.


Inaarifiwa kuwa kushindwa kusonga mbele kwa klabu hiyo katika hatua ya mtoano ya michuano mikubwa ya vilabu barani Ulaya, kunaelezewa kuwa ni sababu kubwa ya kuitia hasara klabu hiyo.


Hata hivyo kiasi hicho kina ashiria maendeleo makubwa kulinganisha na msimu uliopita ambapo City ilipoteza jumla ya euro milioni 243.


Wakati huo huo klabu hiyo imechapisha ongezeko la mapato ya getini na mapato ya malipo ya TV, ambayo kimsingi yameongezeka mara mbili kutoka euro milioni 80 mpaka euro milioni 148.


Kiasi hicho cha fedha sasa kinairuhusu klabu hiyo bingwa nchini England kujiamini kiuwezo kukabiliana na sheria ya shirikisho la soka barani Ulaya( UEFA) ambayo inasimamia udhibiti wa matumizi yasiyopelekea hasara ya kiwango kisichozidi  euro milioni 18.4.

No comments:

Post a Comment