Kocha mpya
wa klabu Simba Patrick Liewig ameutaka uongozi wa klabu ya Simba kumsajili
mshambuliaji kutoka nchini Camerron ambaye jina na wasifu wa mshambuliaji huyo umewasilishwa katika uongozi wa klabu hiyo.
Akiongea na
Rockersports afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kocha Liewig katika
kuhakikisha Simba inafanya vizuri katika michuano ya vilabu barani Afrika
amewataka kumsajili mshambuliaji huyo ambaye anaamini ataisaidia Simba.
Hata hivyo
Kamwaga hakuwa tayari kumtaja mshambuliaji huyo na klabu anayotoka lakini
ameihakikishia Rockersports kuwa uongozi wa Simba kupitia kamati yake ya
usajili chini ya Zakaria Hans Pope uko katika hatua nzuri kumleta mshambuliaji
huyo nchi ambaye pia anatarajiwa kuziba pengo la mshambuliaji raia wa Zambia
aliyeondoka Felix Sunzu.
“Yah ni
kweli Patrick Liewig aliwataka washambuliaji wawili majina tunayo, na sasa
uongozi wa Simba kupitia kamati ya usajili chini ya Hans Pope wanaendelea na
mchakato, tatizo hapa ni kwamba dirisha dogo linafungwa kesho(leo) hivyo bado
tunaangalia sheria za dirisha dogo zikoje? Lakini kamati yetu ya usajili
imeshawasiliana na mmoja wa washambuliaji hao”
“Tunaamini watakuwa ni wachezaji wazuri kwa mujibu wa
taarifa ambazo kocha ametupatia, na namna ambavyo kamati inavyo shughulikia”
Kocha mpya
Patrick Liewig anatarajiwa kuwasili nchini baada ya sikukuu ya Chrismass,
ambapo atasaini mkataba rasmi, tayari kuanza kuifundisha klabu hiyo
yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi.
No comments:
Post a Comment