KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, January 31, 2013

FAINALI MATAIFA YA AFRIKA: TOGO IMEFUZU BAADA YA SARE YA 1-1 NA TUNISIA. TUNISIA NA ALGERIA NJE.

 Extended stay: Tottenham will be without Emmanuel Adebayor for a little longer after Togo made the knockout stages for the first time

Timu ya taifa ya Togo imefanikiwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kwenda sare ya bao 1-1 na Tunisia na kumfanya mshambuliaji wa Totternhan Emmanuel Abebayor kuendelea kukosekana katika timu yake hiyo.
Mwamuzi kutoka nchini Afrika kusini Daniel Bennett aliwazadia penati mbili Tunisia katika mchezo huo uliopigwa Nelspruit kiasi kuibua malalamiko.
Khaled Mouelhi wa Tunisia alipiga penati iliyosaidi Tunisia kusawazisha na kufanya matokeo kusomeka 1-1 kunako dakika ya 30 lakini alishindwa kufunga penati ya pili iliyogonga mwamba na kuigharimu Tunisia kushindwa kuvuka kwa hatua ya robo fainali.
Contrasting emotions: Dejected Tunisian player Zouhair Dhaouadi can only look on as Floyd Ayite gets Togo's celebrations underway
Zouhair Dhaouadi (kulia) akimuangalia Floyd Ayite wa Togo akishangilia baada ya Togo kuandika bao la utangulizi.
Inconsolable: Tunisia's Khaled Mouelhi is distraught as goalkeeper Farouk Ben Mustapha tries to comfort him. Mouelhi missed a penalty with 12 minutes left that would have taken them through
Khaled Mouelhi akijilaumu baada ya kukosa penati zikiwa zimesalia dakika 12.

Serge Gakpe aliifungia Togo bao la utangulizi kunako dakika ya 13 baada ya kazi nzuri ya Emmanuel Adebayor.

Crucial moment: With Togo goalkeeper Kossi Agassa diving the wrong way, Tunisia's Khaled Mouelhi saw his penalty cannon back off the post
Mlinda mlango wa Togo Kossi Agassa akichumpa upande mwingine kufuatia penati ya Khaled Mouelhi wa Tunisia iliyogonga mwamba.
Appeal: Adebayor urges the referee to give a penalty as he's brought down by Tunisian goalkeeper Moez Ben Cherifa
Emmanuel Adebayor akiomba penati kwa mwamuzi baada ya kuangushwa na mlinda mlango Moez Ben Cherifa.
 Togo saa watakutana na Burkina Faso katika hatua ya robo fainali mjini Nelspruit jumapili.

No comments:

Post a Comment