Hatma ya nani kati ya Real
Madrid na Barcelona ataingia katika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la mfalme
(Copa del Rey) sasa itategemea mchezo wa mkondo wa pili februari 26 katika dimba la Camp Nou, baada ya timu hizo hii leo kutoshana nguvu katika mchezo uliopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu.
Timu zote hii leo zilitengeneza nafasi nyingi za kufunga katika kipindi cha kwanza lakini goli la kwanza lilipatikana kunako dakika ya 5 ya kipindi cha pili pale ambapo Cesc Fabregas
alipounasa mpira wa kuetengenezwa na Lionel Messi na kupiga mpira uliompita past Diego Lopez.
Madrid
ilisazisha dakika 9 kabla ya filimbi ya mwisho lililofungwa na Raphael Varane kwa kichwa ya krosi ya Mesut Ozil.
Raphael Varane (kushoto) akishangilia baada ya kufunga bao la kusawazisha.
Habari njema ni kwa kocha wa Madrid Jose
Mourinho kumjumuisha kwa mara ya kwanza kikosini mlinda mlango Lopez aliyejiunga wiki na klabu hiyo wiki iliyopita akitokea Sevilla kuziba pengo la mkongwe Iker Casillas.
Lakini mlinda mlango namba mbili Jose Manuel Pinto akidaka kwa mara ya kwanza na akifanikiwa kuzuia michomo mbalimbali iliyoelekezwa langoni kwake.
Lakini mlinda mlango namba mbili Jose Manuel Pinto akidaka kwa mara ya kwanza na akifanikiwa kuzuia michomo mbalimbali iliyoelekezwa langoni kwake.
Cesc Fabregas akifunga goli la kuongoza la Barcelona.
Fabregas akishangilia goli alilofunga.
Hapa Fabrigas anapongezwa baada na Xavi. |
Varane akipiga kichwa mpira uliozaa goli la kusawazisha la Madrid.
No comments:
Post a Comment