Mshambuliaji wa Simba
Felix Sunzu hii leo anatarajiwa kuwepo katika orodha ya wachezaji watakao
itumikia timu hiyo katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo utakao pigwa
uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam Baada ya
kuwa nje kwa kipindi kirefu akijiweka fiti.
Nafasi ya Sunzu kuwepo
kikosini hii leo inakuja kufuatia mshambuliaji huyo raia wa Zambia
kufanya vizuri katika mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Mbeya City
uliofanyika mkoani Mbeya.
Msemaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga
amesema kiwango kilicho onyeshwa na Sunzu katika mchezo huo ambao mwalimu
Patrick Liewig aliwatumia wachezaji wengi wa kikosi cha pili Sunzu alionyesha
kiwango ambacho kimempa matumaini makubwa mwalimu huyo ya kuanza kumuamini na
kumpa nafasi ya kucheza.
Kiwango cha Sunzu katika siku za hivi karibuni
mimeporomoka sana kutokana na kukabiliwa na maradhi ambayo yamemfanya kupigania
afya yake kwa kipindi kirefu na sasa anaonekana kuwa ameaanza kuwa fiti.
Wakati hayo yakiwa hivyo, naye mlinzi tegemeo wa
kati wa Simba Shomari Kapombe licha ya kuelezwa kuwa hali yake imeanza
kuimarika kufuatia kupata matibabu ya kuondoa damu iliyovilia katika mishipa
yake ya damu.
Hata hivyo mlinzi huyo wa hatakuwepo katika kikosi
cha leo cha Simba kitakacho kuwa kikicheza dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na
kwamba bado yuko katika uangalizi wa daktari wa Simba.
Hata hivyo Kamwaga amesema huenda mchezaji huyo
akaanza kuingia dimbani katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Libolo ya Angola
mchezo utakaochezwa Machi 2 jijini Luanda.
Mussa Mudde ambaye alikuwa kwao nchini Kenya
amerejea jana na kujiunga na kambi ya klabu ya Simba.
Mudde alikwenda kwao kwa ajili ya kushiriki
mazishi ya mwanae.
Hata hivyo nafasi ya Mudde kucheza mchezo wa leo
dhidi ya Mtibwa haipo kufuatia uongozi wa Simba kumpa chaguo kama angependelea
kufanya hivyo ama la kwa kuwa suala la kufiwa na mtoto lipewa uzito mkubwa na
uongozi huo.
No comments:
Post a Comment