Macho na masikio ya wapenzi wa soka nchini yanaelekezwa katika dimba la Old Trafford hapo kesho na pengine yakaelekezwa zaidi kwa mshambuliaji na nahodha wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, ambaye atakuwa akirejea katika uwanja huo kwa mara ya kwanza tangu aihame klabu hiyo kwa uhamisho wa gharama ya rekodi ya dunia ya pauni milioni £80.
Hii leo kikosi kizima cha Real Madrid
kilikuwa kikifanya mazoezi ya mwisho kabla ya pambano hilo la kesho ambapo meneja wa Madrid Jose Mourinho amefanya maamuzi yasiyokuwa ya kawaida ya kufanya mazoezi katika dimba Etihad ambalo linamilikiwa na wapinzani wakubwa wa United, Manchester City, badala ya kutumia uwanja wa utakao tumika kwa mchezo huo wa Old
Trafford.
Pichani juu anaonekana Cristiano Ronaldo akifanya mazoezi siku moja kabla ya kukabilinana na United ambayo ni klabu yake ya zamani kabla ya kuihama.
Real katika kipindi cha majira ya kiangazi walikuwepo katika uwanja huo wa Etihad ambapo walifanikiwa kukiondosha kikosi cha Roberto Mancini katika michuano hiyo ya vilabu bingwa Ulaya.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari bosi wa United Sir Alex Ferguson alisita kuzunguzia juu ya mchezaji gani anadhani atakuwa hatari katika kikosi cha Madrid.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari bosi wa United Sir Alex Ferguson alisita kuzunguzia juu ya mchezaji gani anadhani atakuwa hatari katika kikosi cha Madrid.
Nyota wa zamani wa Liverpool Xabi Alonso ni mchezaji anayetazamwa kama sura ya mchezaji anayefahamika vema kwa United.
No comments:
Post a Comment