Sergio
Busquets amesema taifa kubwa linaelekea kushindwa kufuzu kwa ajili ya fainali
ya kombe la dunia 2014 wakati huu ambapo kikosi cha Vicente del Bosque kikiwa
katika maadnalizi kukutana dhidi ya Ufaransa mchezo mgumu kabisa ambao utapigwa
katika jiji la Paris.
Kufuatia Ufaransa
kushinda dhidi ya Georgia na kisha Hispania kwenda sare dhidi ya Finland ijumaa
iliyopita, mabingwa hao watetezi wa taji wamejiweka pabaya katika msimamo wa
kundi I wakiwa nyuma kwa alama mbili toka kwa Ufaransa maarufu kama Les Bleus.
Licha ya
kwamba watakuwa wamesaliwa na michezo mitatu mara baada ya mchezo wa Paris, bado
majaaliwa ya kufuzu yatategemea na nani atakae kuwa amekalia usukani wa kundi
lakini nafasi ya upendeleo ya moja kwa moja kwa ajili ya fainali hizo.
Kiungo wa Barcelona
Busquets mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kushika dimba la Hispania baada ya
matokeo ya sare ya mwezi Oktoba mjini Madrid ambapo anasema anamatumaini kuwa
kikosi hicho cha Didier Deschamps hakiwanyimi usingizi kuelekea mchezo wa
Jumanne.
Akiongea na
Le Parisien amesema
"Timu
nyingi zinabadilisha mbinu za uchezaji dhidi yetu" wakati mwingine inakuwa
ni kama kukamiana”
Vilanova kurejea Barcelona baada ya kansa nchini Marekani.
Kocha wa Barcelona
Tito Vilanova anatarajia kurejea nyumbani wiki hii baada ya mwezi mmoja wa
matibabu ya kansa inayomsumbua.
Kocha huyo
mwenye umri wa miaka 44 alikuwa akipatiwa matibabu jijini New York nchini
Marekani baada ya kugunduliwa kuwa bado anasumbuliwa na tezi zenye madhara ya kusababisha kansa baada ya kufanyiwa uchunguzi mwezi Desemba.
Msaidizi wake
Jordi Roura, amekuwa akishikilia nafasi yake ambapo taarifa ya klabu hiyo
kupitia mtandao wa klabu hiyo imesema kurejea kwake haimaanishi kuwa atakuwa
anarejea moja kwa moja katika benchi la ufundi la klabu hiyo.
Michezo ijayo
ya Barcelona watakuwa wakikabiliana dhidi ya Celta Vigo jumamosi ukiwa ni
mchezo wa ligi kuu ya nchini Hispania kabla ya mchezo wa Jumanne dhidi ya Paris
Saint-Germain mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya.
Vilanova amekuwa
karibu na klabu yake hiyo katika kipindi chote alichokuwa hayupo ambapo amekuwa
akifuatialia mazoezi kupitia njia ya TV na kuwasiliana na benchi la ufundi
wakati wa michezo mbalimbali kwa njia ya simu.
Ronaldo kwenda Azerbaijan licha ya kuwa na kadi mbili za njano.
Nahodha wa
timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuelekea Azerbaijan pamoja
na kikosi kizima cha timu hiyo kwa ajili ya mchezo wa Jumanne wa kuwani kufuzu kwa
fainali ya kombe la dunia licha ya kwamba mshambuliaji huyo kwasasa anatumikia
adhabu ya kusimama mchezo mmoja.
Mshambuliaji
huyo wa Real Madrid alikuwepo ndani ya dakika zote 90 za mchezo uliopita dhidi
ya Israel mchezo uliofanyika Ijumaa na kumalizika kwa matokeo ya sare ya mabao
3-3 lakini alijikuta akiadhibiwa kwa kadi ya pili ya njano baada ya kucheza ndivyo
sivyo na hivyo kuukosa mchezo huo huko Baku.
Hali
hiyo inaweka uwezekano wa kurejea kwake mapema katika jiji la Madrid kujiandaa
na mchezo wa ligi dhidi ya Real Zaragoza na baadaye kuelekea katika mchezo
dhidi ya Galatasaray ukiwa ni mchezo wa ligi ya mabingwa katika dimba la Santiago
Bernabeu April 3.
No comments:
Post a Comment