Audley Harrison akionekana pichani kushoto wakati akishinda Prizefighter mwezi Februari.
|
Audley Harrison amekubali kuzichapa dhidi ya bondia wa uzito wa juu kutoka nchini Marekani Deontay Wilder pambano ambalo litachezwa April 27 mjini Sheffield.
Harrison mwenye umri wa miaka 41 anarejea ulingoni baada ya kumchapa David Price na kushinda Prizefighter kwa mara ya pili mwezi uliopita.
Hata hivyo Wilder atataka kudhihirisha kuwa yeye ni mkali baada ya kuwa na rekodi ya ushindi wa mapambano 27 mpaka sasa.
Wilder
alikuwa akitajwa kwa muda mrefu kuwa huenda atakuwa bingwa mpya wa uzito wa juu lakini ameshindwa kufanya tangu aingie katika ngumi za kulipwa miaka minne iliyopita.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 27 alipigana kwa mara ya kwanza nje ya ardhi ya Marekani mwezi Januari ambapo alicheza dhidi ya Matthew Greer wa Mexico na kumtwanga na tangu wakati huo amekuwa havuki raundi ya nne.
Amir Khan juu kushoto atakuwa ndiye habari ya siku hiyo huko Sheffield katika pambano kuu dhidi ya Julio Diaz.
TALE OF THE TAPE
Audley Harrison
Born: London
Age: 41
Height: 6’ 5 1/2”
Weight 234lb
Record 31(23)-6
Nickname: A-Force
Born: London
Age: 41
Height: 6’ 5 1/2”
Weight 234lb
Record 31(23)-6
Nickname: A-Force
Deontay Wilder
Born: Alabama
Age: 27
Height: 6’ 7”
Weight 240lb
Record 27(27)-0
Nickname: The Bronze Bomber
No comments:
Post a Comment