Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima amesema timu ya Yanga iko vizuri sana kwasasa tayari kwa mchezo wa jumamosi dhidi ya watani wao Simba na kwamba kinachosubiriwa ni siku ifike na mashabiki waweze kushuhudia karamu yao ya magoli dhdi ya Mnyama. |
Wakati Simba ikijifua katika kisiwa cha
Unguja , timu ya Yanga nayo iko kisiwa cha Pemba ikijifua kujiandaa na
pambano lao na watani wao wa jadi Simba hapo siku ya Jumamosi.
Amekaririwa na Rockersports akitoa maneno haya
"mwili unataka, roho inataka na akili inataka kuwafunga Simba kwa idadi kubwa ya mabao tukishirikiana kama timu kwa kuwa tuko fiti kila idara"
Niyonzima amesema kuwa maandalizi yao ya huko Pemba yanawakumbusha wakati walipokuwa safarini nchini Uturuki wakijiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuun kwamba wachezaji waliiva kiasi cha kutisha na kwamba Pemba kumetulia na kumewakumbusha kambi ya Uturuki.
Amesema kila mtu ana ari kuanzia kocha mkuu wa Ernie Brandts na msaidizi wake Freddy Felix Minziro wamekuwa wakiwakimbusha majukumu yao kila mmoja kwa nafasi yake.
Kwa upande wake mshambuliaji Gerson Tegete amesema kambi yao haina wasiwasi na kwamba wanachama na wapenzi wa Yanga wasiwe na wasiwasi na mchezo huo kwani watahakikisha wanawakabidhi kombe na zawadi ya ushindi dhidi ya Simba msimu huu.
"Timu ikovizuri na tunaendelea vizuri na mazoezi na mashabiki na wanachama wasubiri zawadi ya ushindi dhidi ya mtani baada ya kuwapa kombe"
Pichani juu kabisa: Kiungo wa Yanga , Haruna
Niyonzima akihojiwa na waandishi wa habari, Suleiman Rashid Omar na
Is-hak Mohammed wakati wakiwa katika mazoezi makali ya kutaka kulipiza
kisasi cha kufungwa 5-0 na Simba, kiwanja cha Gombani , Chakechake
Pemba.
Picha ya chini ni kwa hisani ya mtandao wa Yanga wakati wa mazoezi hapo jana.
No comments:
Post a Comment