KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, July 20, 2013

Baada ya Vilanova kushindwa kuendelea na kazi Barcelona Kocha Joan Francesc Ferrer huenda akachukua nafasi yake.

Tito Vilanova speaks to his players during a training session on Thursday
Tito Vilanova ametangaza kuachana na kazi ya kuifundisha Barcelona ili kupata nafasi ya kuendelea na matibabu yake ya kansa hii ikiwa ni taarifa iliyothibitishwa na Rais wa klabu hiyo Sandro Rosell.
Vilanova, ambaye alichukua nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake Pep Guardiola kiangazi iliyopita aligundulika kuwa na kansa mwishoni mwa mwaka 2011, na kuendelea kusumbuliwa na maradhi hayo baadaye.
Alifanyiwa upasuaji mwezi Desemba kabla ya kuanza matibau ya chemotherapy na radiotherapy mjini New York nchini Marekani.

Taarifa kupitia mtandao wa klabu ya Barcelona imesema 
'Tito Vilanova hataendelea kuwepo katika benchi la klabu ya Barcelona.
'Rais Sandro Rosell ametangaza Ijumaa hii kuwa kocha huyo wa Katalunya hataanza msimu na klabu'

Katika mkutano uliochukua muda mfupi uliohudhuriwa na wachezaji Rosell ametanabaisha kwa kusema,
'Taarifa niliyonayo ni kitu ambacho msingependa niwaeleze.
'Baada ya kufuatilia hali ya Tito na mwendelezo wa matibabu yake ni kwamba matibabu yatakayo fuatia yatakuwa yanamuweka katika wakati mgumu kuendelea kuwa kocha wa kikosi cha kwanza.
'Nataka niwaelezea kwa heshima juu ya unyeti wa mchakato wake.'
'Ni pigo kubwa lakini Barca imeshawahi kupatwa na mapigo mengi ' 
Ameongeza Rosell kwa kusema klabu hiyo inatarajia kutangaza mbadala wa Vilanova katika siku zijazo.
Sad affair: Sandro Rosell and Andoni Zubizarreta have confirmed Vilanova's departure
Sandro Rosell na Andoni Zubizarreta wamethibitisha kuondolewa kwa Vilanova.

Taarifa kutoka nchini Hispania zinasema kuwa huenda Joan Francesc Ferrer, maarufu kama Rubi, huenda akachkua nafasi hiyo ya Vilanova.

Rubi mwenye umri wa miaka 43 alijunga na Barca kama mmoja wa makocha wa Barca mwezi uliopita akiwa msaidizi wa Vilanova na Jordi Roura ambaye alikuwa akiziba nafasi ya Vilanova pale alipokosekana.

Rubi alikuwa mkuu wa Girona msimu uliopita ambayo aliiongoza katika michezo ya ligi ya Segunda Division, ambapo walifungwa na Almeria na kukosa nafasi ya juu kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo.
Rubi aliiingia mkataba wa mwaka mmoja na Barca kwa masharti ya kuweza kuongeza katika msimu utakao fuata na kaunza kazi mapema wiki hii na akitarajiwa kuunga na kikosi mara baada ya michezo ya pre-season.
Haijatajwa wazi nani atakuwa mrithi wa Vilanova lakini alikaririwa Rosell akisema : 
'Siku chache zijazo makamu wa Rais Josep Maria Bartomeu na mkurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta watatangaza kocha mpya pengine mapwema wiki ijayo.'
Tough task: Rosell will have to find a replacement for VilanovaInfluential: Key players like Lionel Messi could be affected by the manager's departure
Ill health: Vilanova has suffered a relapse
In the frame: Coach Joan Francesc Ferrer could take over
Kocha Joan Francesc Ferrer huenda akachukua nafasi yake.

No comments:

Post a Comment