Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski bado anaoenakana ni mwenye hasira
moyoni kutokana na hatua ya klabu yake kukataa kumruhusu ajiunge na
mabingwa wa mataji matatu msimu uliopita Bayern Munich.
Lewandowski anasema hawezi kuficha ukweli kwamba anahisi alisalitiwa kwa
sababu maafisa wa klabu yake walishindwa kabisa kukubaliana na mazungumzo yao ya awali na kwenda kinyume na jinsi walivyokubaliana.
Lewandoswki amesema Dortmund walivunja ahadi yao wakati walipokataa
kumruhusu aondoke hadi mkataba wake utakapokamilika mwaka wa 2014 na
kwamba nyongeza kubwa ya mshahara aliyoahidiwa kupewa katika msimu huu
unaoanza bado haijaanza kutekelezwa.
Nyota huyo wa Poland hata hivyo ameahidi kufanya kila awezalo
kuhakikisha kuwa Dortmund wanashinda mataji zaidi msimu huu, ijapokuwa
anasema hajui kama hali ya sasa itaathiri mchezo wake. Kocha wa BVB
Jurgen Klopp amesema kwamba klabu hiyo itafanya mkutano na Lewandowski
ili kulitatua suala hilo kabla ya kuanza msimu mpya.
Emre Can ahamia Leverkusen kutoka Bayern
Emre Can ni mmoja wa wachezaji chipukizi wenye vipaji katika soka la Ujerumani |
Wakati hayo yakiwa hivyo msimu huu wa majira ya kiangazi tayari umeshuhudia kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani ya wachezaji walio na umri wa chini
ya miaka 21 Emre Can amehama klabu ya Bayern Munich na kujiunga na
klabu ya Bayer Leverkusen kwa kusaini mkataba wa miaka minne.
Huku Bayern ikiwa na wachezaji kumi viungo wa kimataifa, Can mwenye umri
wa miaka 19 hakuhakikishiwa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza
chini ya kocha mpya wa Bayern Pep Guardiola na hivyo anajiunga na
Leverkusen ambao walifuzu moja kwa moja katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Bayern wana chaguo la kumnunua tena atakapokamilisha mkataba wake katika
klabu ya Leverkusen.
No comments:
Post a Comment