Wakati msimu mpya wa kandanda barani Ulaya unakaribia kuanza, nchini
Ujerumani shughuli inaanza rasmi, kwa mechi za duru ya kwanza ya kombe la
Shirikisho.
Michezo hizo linazishirikisha timu kutoka ligi kuu Bundesliga hadi za
daraja ya sita, na kama kawaida matokeo ya kushangaza hayakosekani.
Mechi 32 zinachezwa
wikendi hii. Katika michezo ya mwaka jana, timu sita za Bundesliga
ziliangushwa na timu za daraja za chini katika duru ya kwanza.
Kila mtu
atakuwa akisubiri kuona nani atachuana na nani,
kuna yule atakayeweka historia na mashabiki wa soka wa Ujerumani
watapata fursa ya kujua majina mengine kadhaa mapya katika kandanda.
Fainali ya michuano hiyo kama kawaida huwa inaandaliwa katika uwanja wa
Olimpiki mjini Berlin mwezi Mei.
Matokeo ya leo
Finished
|
Magdeburg
| - |
Cottbus
| (0-0) | ||||||
Finished AET
|
TSG Neustrelitz
| - |
Freiburg
| (0-0) | ||||||
Finished
|
Wilhelmshaven
| - |
Borussia Dortmund
| (0-0) | ||||||
Finished
|
Bahlinger SC
| - |
Bochum
| (0-2) | ||||||
Finished
|
Fortuna Koln
| - |
Mainz 05
| (1-1) | ||||||
Finished
|
Lippstadt
| - |
Bayer Leverkusen
| (1-3) | ||||||
Finished
|
Neckarsulmer Sport Union
| - |
Kaiserslautern
| (0-2) | ||||||
Finished
|
SG Aumund-Vegesack
| - |
Hoffenheim
| (0-0) | ||||||
Finished
|
Sportfreunde Baumberg
| - |
Ingolstadt
| (0-2) | ||||||
Farasi wawili tena nchini Uhispania?
Mchuano wa El Classico baina ya Barcelona na Real Madrid hutazamwa na mamilioni ya mashabiki kote ulimwenguni
Nchini Uhispania, bado zimesalia wiki mbili kabla ya ligi kuu
ya La Liga kuanza, na tayari huenda ikawa rahisi kutabiri ni timu zipi
zitamaliza katika nafasi ya kwanza na pili.
Tangu mwaka wa 2008,
Barcelona na Real Madrid zimekuwa zikimaliza katika nafasi mbili za
kwanza, huku Barca ikishinda mataji manne ya ligi nayo Real moja katika
misimu mitano iliyopita.
Kitu ambacho hakijulikani ni kama kocha mpya wa Real Carlo Ancelotti
ataweza kubadilisha mambo, au kama kocha mpya wa Barca Gerardo Martino
ataibakisha klabu hiyo kileleni.
Vilabu hivyo viwili vimekuwa
vikinufaika zaidi na fedha za haki ya matangazo ya televisheni kuliko
vilabu vingine nchini Uhispania.
Barca na Real wawasajili nyota wapya
Wakati Barca wakiimarisha safu yao ya mashambulizi kwa kumsajili nyota
wa Brazil Neymar, na wakati Real wakitarajiwa kuvunja rekodi ya uhamisho
kwa kumsajili nyota wa Wales Gareth Bale, vilabu vingine vyote
vimelazimika kuwa na wachezaji wao.
Atletico Madrid, ambao walimaliza wa tatu msimu uliopita na kisha
wakawashinda Real katika fainali ya kombe la Mfalme, wamemmuuza
mshambuliaji wao nyota Radamel Falcao kwenda AS Monaco. Real Soceidad
ambao walimaliza wa nne wamemuuza kiungo Asier Illaramendi katika klabu
ya Real wakati nambari tano Valencia wakimuuza nahodha Roberto Soldado
katika klabu ya Tottenham Hotspur.
Kuondoka kwa Soldado kuna maana kuwa wafungaji mabao mengi katika La
liga msimu uliopita, Falcao, Negredo na Soldado wote wamehama ligi hiyo.
Pia mshambuliaji wa Uhispania Fernando Llorente ameihama Athletic
Bilbao na kujiunga na Juventus. Hao ni wachache na kuna wengi ambao wamehama kutoka upande mmoja na kwenda upande mwingine.
Ratiba ya ligi ya Hispania mwezi huu itakuwa kama ifuatavyo.
Saturday, 17 August 2013
Real Sociedad v Getafe, 18:00
Valladolid v Athletic Bilbao, 20:00
Valencia v Malaga, 22:00
Sunday, 18 August 2013
Barcelona v Levante, 18:00
Osasuna v Granada, 20:00
Real Madrid v Real Betis, 20:00
Sevilla v Atletico Madrid, 22:00
Monday, 19 August 2013
Rayo Vallecano v Elche, 19:00
Almeria v Villarreal, 21:00
Celta de Vigo v Espanyol, 21:00
Friday, 23 August 2013
Getafe v Almeria, 19:00
Athletic Bilbao v Osasuna, 21:00
Saturday, 24 August 2013
Elche v Real Sociedad, 18:00
Espanyol v Valencia, 20:00
Villarreal v Valladolid, 22:00
Sunday, 25 August 2013
Atletico Madrid v Rayo Vallecano, 18:00
Levante v Sevilla, 20:00
Malaga v Barcelona, 20:00
Real Betis v Celta de Vigo, 22:00
Monday, 26 August 2013
Granada v Real Madrid, 20:00
No comments:
Post a Comment