Burkina Faso itafanya maandalizi yake nchini Belgium kuelekea katika mchezo wa marudiano wa hatua ya mtoano mtoano dhidi ya Algeria mwezi ujao.
Shirikisho la soka la nchi hiyo limesema hii leo kuwa Stallions itakuwa na maandalizi ya siku tano mjini Brussels kuanzia Novemba 10 kabla ya kusafiri kuelekea katika jiji la Algiers tayari kwa mchezo huo.
Timu hizo zitakuwa uwanjani Novemba 19 katika mji wa Blida, kiasi cha kilometa 50 kutoka katika mji mkuu wa Algiers.
Maafisa wa Burkinabe wamesema mashabiki wake hawatasafiri kuelekea katika mchezo huo kwa kukwepa ghasia kutoka kwa mshabiki wa Algeria.
Washindi hao wa pili wa michuano ya mataifa ya Afrika walishinda 3-2 katika mchezo wao wa kwanza uliopigwa Ouagadougou mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment